Wajumbe wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania(ALAT)
Mkoa wa Ruvuma wakikagua mradi wa vyanzo vya Maji vilivyopo katika mlima
Matogoro mjini Songea,
Wajumbe wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania(ALAT)
Mkoa wa Ruvuma wakikagua mradi wa Kibanio cha umwagiliaji katika kata ya Subila
iliyopo Manispaa ya Songea
Banio hili limegharimu kiasi cha Tshs Milioni Mia
mbili ishirini hadi kufikia hapa lilipo.
Wajumbe wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania(ALAT)
Mkoa wa Ruvuma wakiwa katika kituo kikuu cha mabasi kinachojengwa katika eneo la
Msamala kwa mfumo wa JENGA ,ENDESHA,KABIDHI.
Mfumo huu unamuwezesha mwananchi kujenga kibanda
nakukitumia kwa mkataba wa miaka kumi na moja kisha anakabidhi halmashauri ya
Manispaa ya Songea.Hata hivyo wajumbe walihoji juu ya ujenzi huo na ukubwa wa
eneo kulingana na ongezeko la watu, magari na huduma nyinginezo katika eneo hilo
kuwa haliwezi kukidhi ongezeko hilo kutokana na eneo hilo kuonekana
dogo.
Wajumbe wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania(ALAT)
Mkoa wa Ruvuma wakiendelea kuhoji juu ya ujenzi wa kituo hicho kipya cha Mabasi
ambacho kimezua utata miongoni mwa wajumbe hao.
Toka kushoto ni katibu wa ALAT mkoa wa Ruvuma Mohamedi
Maje akiwa na mjumbe kutoka wilayani Tunduru wakiwa wameshikwa na butwaa baada
ya taarifa ya utekelezaji wa ujenzi wa kituo hicho cha
Mabasi
Kaimu Mhandisi wa Manispaa ya Songea Davis Mbawala
akijibu maswali ya wajumbe juu ya ujenzi wa kituo kipya cha mabasi kinachojengwa
kwa mfumo wa JENGA,ENDESHA,KABIDHI,
Toka kulia ni Naibu Meya wa Manispaa ya Songea Wiloni
Kapinga, Mwandishi wa habari wa ALAT mkoa wa Ruvuma Nathan Mtega na mkurugenzi
wa Halmashauri ya Namtumbo ambaye pia ni Katibu wa ALAT mkoa wa Ruvuma Mohamed
Maje wakiwa katika picha ya pamoja
Katibu wa ALAT mkoa wa Ruvuma Mohamed Maje akiteta
jambo na Naibu Meya wa Manispaa ya Songea Wiloni Kapinga wakati wa majumuisho ya
ziara ya wajumbe wa ALAT baada ya ukaguzi wa miradi
Wajumbe wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania(ALAT)
Mkoa wa Ruvuma wakiwa ndani ya ukumbi wa mkutano
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Tunduru akitoa
hoja katika kikao cha majumuisho baada ya ziara ya kukagua
miradi
Mwandishi wa habari Cresencia Kapinga akitoa
mapendekezo katika kikao cha majumuisho.
Mkurugenzi wa halmashauri ya Tunduru Robert Nehata
akiuliza swali
katibu ALAT Mohamed Maje akizungumza kabla ya
kumkaribisha mwenyekiti wa ALAT Mkoa wa Ruvuma Oddo Mwisho
CREDITS: DEMASHO
Post a Comment