Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

WATOTO 18 KATI YA 1000 WENYE UMRI WA CHINI YA MIAKA 5 HUFARIKI IRINGA


 
ured 095 643a9
Mwezeshaji wa Wizara ya afya na ustawi wa jamii, Jamari Soko akitoa ufafanuzi juu ya mafunzo ya ubia kati ya sekta binafsi na sekta ya umma.

IMEELEZWA kuwa watoto 18 katika kila watoto 1,000 wenye umri wa chini ya miaka mitano hufa mkoani Iringa.

Akizungumza na mwandishi wa habari hii kwenye ukumbi wa katibu tawala wa mkoa wa Iringa, Katibu wa afya wa mkoa wa Iringa Adeodatus Mhagama alisema kati ya hao 14 katika kila watoto 1000 wenye chini ya umri wa mwaka mmoja hufa katika wilaya za mkoa wa iringa.
Alisema takwimu hizo ni ndogo ikilinganishwa na zile za kitaifa jambo linaloashiria hali ya utoaji wa huduma za afya kwa mkoa wa Iringa si mbaya sana.
Pia aliongeza kuwa kwa upande wa akinamama wajawazito Mhagama alisema 223 kati ya akinamama 100,000 hufa kutokana na matatizo mbalimbali ya uzazi.
Alizitaja sababu ya vifo hivyo kwa watoto na wajawazito kuwa ni pamoja na malaria, kutokwa na damu nyingi wakati wa kujifungua, UKIMWI, motto kulala vibaya na mtoto kupata maambukizi wakati mama anapojifungua.
Alisema hali ya utoaji wa huduma za afya mkoani Iringa ni hospitali nne za binafsi na tatu za serikali, vituo vya afya 21 na zahanati 226.
Naye Mkufunzi wa mafunzo kutoka wizara ya Afya, Jamari Soko alisema kitaifa sekta binafsi inamiliki hospitali 137 kati ya 240 zilizopo, vituo vya afya 189 kati ya 633 na zahanati 1,412 kati ya 5,469 zilizopo nchini.
Kwa mkoa wa Iringa kuna vituo 254 zikiwemo hospitali saba, vituo vya afya 21 na zahanati 226 na kuwa taasisi binafsi imejikita zaidi maeneo ya mijini katika hospitali wakati serikali iko katika maeneo mengi ya vijijini hasa vituo vya afya na zahanati.

Alisema changamoto iliyopo ni kuongeza zaidi vituo vya afya katika maeneo ya vijijini ambapo huduma ya afya imekuwa duni, jambo linalohitaji ushirikiano wa pamoja kati ya sekta binafsi na umma ili kuboresha afya za wananchi. Chanzo: mjengwablog
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top