WAZIRI mkuu Mizengo Pinda amesema udhaifu
mkubwa uliopo katika serikali ni kukosekana kwa umakini wa ufuatiliaji na
usimamizi imara, wa miradi inayoibuliwa kwa lengo la kuwainua wananchi, hali inayosababisha
miradi kutokamilika na dhamani ya fedha kutoendana na miradi.
Pinda ametoa
kauli hiyo jana mjini Moshi, wakati akizinduwa mradi waUimarishaji wa Miji 18
za Tanzania bara, ulifadhiliwa na benki ya dunia kwa lengo la
kuimarisha uwezo wa kutekeleza majukumu ya Halimashauri na miji ili kutoa
huduma bora kwa wanachi.
Alisema tatizo
kubwa lililopo ndani ya serikali ni kukosena kwa ufuatiliaji makini wa miradi,
hali inayosababisha miradi kukamilika chini ya kiwango, pamoja na dhamani fedha
kutoendana na kazi husika.
Amesema baadhi
ya watendaji wa halimashauri wamekuwa mabingwa wa kutafuta visingizio pindi
mradi unaposhindwa kukamilika kwa wakati, au chini ya kiwango, kwa kujitetea
vifaa viliibiwa, na kudai uzembe kama huo
hatokubalina nao katika mradi huu wa miji.
Waziri panda
amesema serikali haitakuwa tayari kusikiliza vigezo wala sababu zozote za
kukwamisha kazi ya mradi huo, wala kufumbia macho uzembe au ubadhilifu wa
fedha au vifaa utakaosababisha kazi kukwama au kutekelezwa chini ya kiwango.
Amesema
litakuwa jambo la kusikitisha na kusononesha endapo itatokea mojawapo ya
halimashauri kati ya 18 zilizochaguliwa, kuishia njiani bila kukamilisha mradi
huo kwa muda wa miaka mitano.
Amebainisha
mradi huo utaongeza imani kwa wananchi na kuvutia wadau wengine kushirikiana na
halimashauri za hapa nchini, hivyo wakurugenzi wanatakiwa kuomba ushauri kwa
viongozi pale wanapoona kuna dalili za vikwazo ambavyo vinaweza kusababisha
ucheleweshaji wa utekelezaji wa mradi.
Pinda amesema
njia ya kufikia mafanikio ya mradi huo ni kuwepo kwa uwajibikaji, utunzani wa
miradi iliyokamilika, ukusanyaji wa mapato, pamoja na ushirikishwaji wa
wananchi kwa kushirikisha ngazi zote ikiwa ni pamoja na taarifa za utekelezaji
wa mradi ziwekwe wazi.
Kwa upande wake
Kaimu Katibu mkuu ofisi ya Waziri mkuu (TAMISEMI), Jumanne Sangini alisema
mradi huo unatekelezwa kwa ufadhili wa benki ya dunia kwa garama ya zaidi ya Sh
bilioni 400 kwa miji ipatayo 18 ya hapa nchini Sangini alisema mradi huo
unalenga kuimarisha halmashauri za miji katika maeneo matano ili ziweze kutoa huduma
bora zaidi kwa wananchi, moja ikiwa ni kuboresha mfumo wa mipango miji na
ukusanyaji wa mapato ya ndani,.
Ametaja maeneo
mengine ya mradi utakapolenga kuwa ni uboreshaji wa mifumo ya udhibiti wa fedha
manunuzi ya maswala ya mazingira, mfumo wa utekelezaji utunzaji wa miundombinu
kwa ajili ya huduma za jamii, na kuboresha uwajibikaji.
Mwandishi: Arnold
Swai, Moshi-Kilimanjaro
Post a Comment