Waziri
wa Nishati na Madini, Mh.Profesa Sospeter M. Muhongo, akimfafanulia
jambo Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Chiyoda Corporation ya
Japan, Bw. Shogo Shibuya. Waziri Muhongo alikutana na Bw. Shogo kwa
lengo la kufanya mazungumzo kuhusu uwekezaji nchini kwenye miradi ya
uzalishaji wa umeme kwa kutumia jua pamoja na ujenzi wa miundombinu ya
usindikaji wa gesi asilia na mitambo ya kuzalisha umeme. Mkutano huo
ulifanyika mjini Yokohama, Japan wakati wa Mkutano wa tano wa Kimataifa
wa Tokyo unaojadili Maendeleo ya Afrika (Tokyo International Conference
on African Development (TICAD V) uliohudhuriwa na Wakuu wa nchi za
Afrika na Japan pamoja na Mawaziri na Maofisa wa Serikali hizo. Mkutano
ulifanyika tarehe 1 hadi 3 Juni, 2013.
Loading...
Home » Unlabelled » Waziri wa Nishati na Madini akutana na Rais wa Kampuni ya Chiyoda Corporation ya Japan
Post a Comment