Hifadhi ya Ruaha ni eneo muhimu sana la kiuchumi kutokana na kuhifadhi maji ya mto Ruaha Mkuu yanayo tumika kwa matumizi ya nyumbani, na kilimo cha umwagiliaji pamoja na uvuvi kwa watu wanao ishi kandokando yake
Mto Mazombe na Ruaha mkuu inatiririsha maji kwenye Bwawa la Mtera na baadae kwenye Bwawa la kidatu ambako umeme unazalishwa kwa ajili ya gridi ya Taifa.
Vivutio vya kitalii vilivyopo Hifadhi ya Raha,
Ndege, Wanyama,Reptilia na Amphibia, Mimea, Maeneo ya kitamaduni,
Mandhari,Mito, Bonde la ufa Chemchemi za maji , Miinuko,
Wakati mzuri wa kutembelea hifadhi,
unaweza kutembelea hifadhi muda wowote lakini kipindi cha masika (mwezi wa tatu na wanne) niwakati mzuri wa kuona ndege maji na maua Wakati wa kiangazi (mwezi wa sita
hadi wakumi na moja) niwakati wa kuona wanyama wengi kandokando ya Mto Ruaha na Mabwawa ya maji yasio kauka mapema kipindi cha kiangazi;
Hifadhi inafikika kwa urahisi kwa kipindi chote cha mwaka mzima kwanjia ya Barabara na ndege kutoka Zanzibar, Dar-es-Salaam,Arusha,Dodoma na Mbeya.Karibuni sana wageni toka nje ya nchi na ndani ya nchi mje mjionee Utalii wetu.Said Ng'amilo Mjengwablog

Post a Comment