Mtuhumiwa wa Kesi
ya kuiba na kughushi Benki Deogratius Mpembe
akisomewa mashitaka
Mtuhumiwa wa Kuiba na
kugushi Deogratius Mpembe akiwa anatoka
mahakamani baada ya kufungwa kifungo cha Miaka 20
Mtuhumiwa wa
Kesi ya Kuiba na Kughushi Benki akiondoka
Mahakamani
**********************
MTU mmoja
aliyefahamika kwa jina la Deogratius Mpembe amehukumiwa kutumikia kifungo cha
Miaka 20 Jela kwa kosa la kughushi nyaraka za kutolea fedha katika Benki ya CRDB
Tawi la Mwanjelwa Jijini Mbeya.
Hukumu hiyo
imetolewa jana na Hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Mbeya Gilbert Ndeuruo, baada
ya kumtia hatiani Mshtakiwa kwa makosa 14 ambayo Mtuhumiwa
alikubali kutenda baadhi ya makosa na mengine
kuyakanusha.
Mwendesha
mashtaka wa Serikali Lugano Mwakilasa aliiambia mahakama hiyo kuwa Mshtakiwa
alitenda makosa hayo katika vipindi tofauti kati ya Mwezi Juni, 2011 kinyume cha
kifungu cha 235 Sura ya 20 ya Mwaka 2002 ya kanuni ya
adhabu.
Mwakilasa alisema
Mtuhumiwa alipatikana na Kosa la kughushi nyaraka za kutolea fedha katika Benki
ya CRDB katika akaunti mbili za mteja wa benki hiyo ambaye ni marehemu Clemence
Kihanga ambaye imedaiwa mahakamani hapo kuwa na uhusiano na
Mshtakiwa.
Mbali na kosa
hilo Mtuhumiwa huyo pia anadaiwa kuiibia Benki hiyo fedha za
kigeni Dolla za Marekani 118,137.4 pamoja na fedha za kitanzania Shilingi Milion
2,468,181.24 ambapo Mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo akiwa ni
karani wa Benki hiyo akiwa na kitambulisho cha kazi chenye namba
CK 4M.
Upande wa
Mashtaka ulikuwa na mashahidi wanne ambao ni Meneja wa benki hiyo tawi la
Mwanjelwa Ephraim Luwila, Mtaalamu wa maandishi kutoka Jeshi la Polisi namba
E2912 Johanes, Mke wa Marehemu Niku Kihanga na Kaimu Meneja wa Benki hiyo Alfred
Basajile.
Katika maelezo
yao Mashahidi hao walitoa Vielelezo mbali mbali mahakamani hapo kama sehemu ya
ushahidi ikiwemo Kitambulisho cha kazi cha Mtuhumiwa, Hati ya Kifo cha marehemu
aliyefariki Novemba 2010 na Nyaraka za maandishi ambazo zote zilikuwa na
miandiko inayofanana na Mtuhumiwa kama vile Mkato na Sahihi
zake.
Awali ilielezwa
kuwa kugundulika kwa wizi wa fedha hizo ni baada ya Mke wa Marehemu Niku Kihanga
kufuatilia masalio ya akiba ya Mume wake baada ya kuidhinishwa kuwa msimamizi wa
mirathi na kuomba kupewa masalio ya akiba zote na kukuta kuna upungufu wa Dola
5000 kwa akaunti ya fedha za nje na akaunti ya ndani ikikutwa na Shilingi
36,000/= badala ya Shilingi 2,400,000/=.
Mke wa marehemu
alisema kufuatia kuwepo kwa upungufu mkubwa wa fedha hizo aliamua kupeleka
malalamiko kwa Meneja wa benki hiyo ambaye alianza kulifanyia kazi kwa kupeleka
malalamiko Polisi.
Kutokana na
Ushahidi huo pamoja na maelezo ya kukiri Polisi,
Hakimu Gilbert Ndeuruo alimtia hatiani Mtuhumiwa kwa makosa yote
14 na kumhukumu kila kosa kwa miaka Mitano ambapo alisema Mtuhumiwa atatumikia
makosa yote kwa pamoja kwa kwenda Jela Miaka
20.
Aidha kabla ya
kutoa hukumu hiyo Mwendesha mashtaka Lugano Mwakilasa aliiomba Mahakama hiyo
kutoa adhabu kali ili iwe fundisho kwa watumishi wengine wasiokuwa
waaminifu.
Hata hivyo Hakimu
huyo kabla ya kutoa hukumu alimtaka Mtuhumiwa huyo kujitetea ili apunguziwe
adhabu ya kifungo cha maisha kutokana na makosa aliyokutwa nayo, ambapo
Mtuhumiwa huyo aliiomba mahakama kumpunguzia adhabu kwa kile alichodai
anasumbuliwa na ugonjwa wa Kansa, Mtoto mmoja, Mkewe na Mdogo wake ambaye
anamsomesha kuwa wanategemea msaada wake.
Pamoja na utetezi
huo ambao Hakimu aliridhika nao na kumpunguzia adhabu kutoka Kifungo cha Maisha
hadi kumfunga kutumikia Jela kwa Miaka 20 na kuongeza kuwa anaruhusiwa kukata
rufaa endapo hatakuwa ameridhika na adhabu aliyopewa ndani ya Siku
30.
PICHA , HABARI NA
MBEYA YETU BLOG
Post a Comment