watu 21 wamejeruhiwa vibaya na wengine 30 wakinusurika
kifo baada ya basi walilokuwa wakisafiria kutoka jijini Dar es salaam kwenda
Songea kupata ajali eneo la vigwaza mkoani pwani.
akizungumza na MCHOME BLOG mkuu wa kikosi cha askari
wa barabarani Chalinze Assistance Inspector Sule amesema ajali hiyo imetokea
majira ya saa mbili asubuhi ya leo July 02 baada ya basi la abiria la kampuni ya
Saibaba lenye namba za usajili T 779BKL kutaka kulipita gari lingine huku likiwa
katika mwendo kasi na hatimaye gari lilimshinda dereva huyo na kisha
kupinduka
Aidha ameongeza kuwa majeruhi hao wamekimbizwa katika
hosiptali ya tumbi kibaha kwaajili ya matibabu,basi hilo lilikuwa na jumla ya
abiria 51.
Habari kwa hisani ya www.mchomeblog.com
Post a Comment