Binti
mmoja nchini Afrika Kusini amenusurika kifo baada ya kumbusu simba
anayefugwa aliyekuwa amefungiwa katika banda lake katika hifadhi ya
wanyamapori nchini humo.
Kijana
huyo Lauren Fagen kutoka Montreal amepata majeraha kadhaa mwilini kwake
wakati Simba huyo dume alipovuta miguu yake ndani ya banda hilo katika
kituo cha Moholoholo Wildlife Rehabilitation.
Lauren Fagen akiwa Hospitalini akiuguza majeraha baada ya kujeruhiwa na Simba huyo.
Binti
huyo mwenye umri wa miaka 18 anayefanya kazi za kujitolea anaye endelea
na matibabu katika hospitali amesema ni bahati kubwa kwake kuwa hai.
Fagen
alianza kazi za kujitolea katika kituo cha wanyamapori mwezi Juni mwaka
huu akifanya usafi katika mabanda ya simba na kuwalisha wanyama
wengine.
Post a Comment