Na Albert G. Sengo
MWANZA.
WAZIRI Mkuu mstaafa Mhe.Edward
Lowassa ijumaa usiku aliongoza harambee kubwa na ya kihistoria ya
kuchangia kituo cha Redio IQRA Fm kinachomilikiwa na Baraza Kuu la
Waislamu Mkoa wa Mwanza (BAKWATA) iliyofanyika katika ukumbi wa Hoteli
ya Gold Crest Jijini Mwanza.
Mhe.Lowassa aliyekuwa Jijini Mwanza kushirikiana na marafiki zake,
wafanyabiashara, taasisi na makampuni mbalimbali, watu binafisi na
viongozi wa serikali na vyama vya siasa na wabunge wa majimbo mawili ya
jijini Mwanza Ilemela na Nyamagana kupitia CHADEMA yaliyotuma
wawakilishi wao hatimaye aliweza kuvuka lengo lililowekwa kwa kukusanya
zaidi ya shilingi milioni 590 zikiwemo ahadi.
Katibu wa BAKWATA mkoa wa Mwanza Shekhe Mohamed Bala akizungumza na hafla hiyo ya harambee kuchangia maboresho ya radio za kiislamu zenye lengo la kutoa elimu zaidi kwa umma. |
"Ninaamini vituo
vya redio Iqra FM na redio Sauti ya Qur-ani kitaonyesha Uislamu kama dira
unayohusisha mambo yahusuyo jamii. Ni cheche ya kimungu ambayo inatoa ubinafsi
pia inayo waunganisha binadamu katika jamii moja. Korani inasema binadamu
ameumbwa kutokana na roho moja, kama mwanaume na mwanamke, jamii na mataifa,
ili watu waweze kufahamiana. Inawaleta watu wa imani zote kwenye jukwaa moja,
kwa kupitia wema."
CHANGIZO LIKAANZA:
CREDITS: GSENGO BLOG
Post a Comment