Balozi
Seif akiangalia ujumbe wa simu aliotumiwa wa kupokea fedha kwa njia ya
huduma ya kusafirisha fedha kwa haraka kutoka kwa mmoja wa Marafiki zake
Bwana Hassan aliyeko Canada kupitia kituo cha huduma cha PBZ kiliopo
Mazizini.
Pembeni yake ni mtendaji wa Kituo hicho cha PBZ Rashid Mohd Hassan akisubiri kuthibitisha ukweli wa Ujumbe huo ili ampatie fedha zake.
Balozi
Seif akifurahia fedha alizotumiwa na Rafiki yake Bwana Hassan aliyeko
Canada baada ya kuzipokea kupitia Kituo cha PBZ kiliopo Mazizini katika
mfumo wa huduma za kusafirisha fedha kwa njia ya haraka.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Benki ya Watu wa Zanzibar Limited Nd. Juma Amour Mohammed
akitoa taarifa katika hafla ya uzinduzi wa Kituo cha kutoa huduma cha
PBZ sambamba na uzinduzi wa huduma za kusafirisha fedha kwa haraka hapo
Mazizini.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akizungumza katika uzinduzi wa
Kituo cha kutoa huduma cha PBZ sambamba na huduma za kusafirisha fedha
kwa haraka hapo katika jengo la Mamlaka ya Mapato Zanzibar { ZRB } Mazizini.
Baadhi
ya Wafanyakazi wa Benki ya Watu wa Zanzibar walioshuhudia uzinduzi wa
Kituo cha kutoa huduma cha PBZ sambamba na huduma za kusafirisha fedha
kwa haraka hapo Mazizini. Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.
*************************************
Mabenki
Nchini yametakiwa kuimarisha eneo la kuhudumia wateja kwa urahisi na
haraka zaidi ili kupunguza malalamiko ya wateja wakati wanapohitaji
huduma za fedha ambazo huwachukuwa muda mrefu kuzipata katika matawi ya
baadhi ya Benki hizo.
Tabia
hiyo huonekana kufanywa na baadhi ya Watendaji wa Matawi hayo kwa
kutokaa kutoa huduma katika sehemu zao za kazi na kuwapa mwanya baadhi
ya watumishi wa Umma kupata kisingizio cha kutoroka makazini.
Wito
huo umetolewa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali
Iddi mara baada ya kuzindua Kituo cha kutoa huduma sambamba na uzinduzi
wa huduma ya kusafirisha fedha kwa haraka { World Remit Money Transfer
Servives } za Benki ya Watu wa Zanzibar { PBZ } katika jengo la Mamlaka
ya Mapato Zanzibar { ZRB } liliopo Mazizini Nje kidogo ya Mji wa
Zanzibar.
Balozi
Seif alisema wakati umefika kwa Benki za Hapa nchini kubadilika kwa
kuweka malengo ya kupunguza muda wa kuhudumia wateja ambao ni wafalme
katika masuala ya kupatiwa huduma.
“
Kuna malalamiko ya wateja wengi nchini kutumia muda mrefu sana
wanapofika kwenye matawi ya Benki zetu. Sasa watendaji wetu umefika
wakati mbadilike mara moja kwa kuweka malengo ya kuondoa usumbufu huo “.
Alisisitiza Balozi Seif.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliupongeza Uongozi wa Benki ya Watu wa
Zanzibar pamoja na watendaji wake kwa kupiga hatua kubwa katika utoaji
wa huduma mbali mbali za Kibenki.
Alisema
uanzishwaji wa huduma za usafirishaji fedha kwa haraka ni kielelezo
kinachodhihirisha kwamba Benki ya Watu wa Zanzibar ni miongoni mwa
Benki kongwe Nchini ambayo inapiga hatua za haraka katika utoaji wa
huduma zake.
Alieleza
kwamba huduma iliyoanzishwa na PBZ ya kusafirisha fedha kwa haraka
kupitia mtandao wa inaternet ni huduma iliyowalenga zaidi Wazanzibari na
Watanzania wanaoishi nje ya nchi waweze kutumia huduma hizo kwa kutuma
fedha kwa ndugu na jamaa zao katika njia ya urahisi na uhakika.
Balozi
Seif alielezea matumaini yake kwamba matumizi ya mtandao huo
yataongezeka hasa kutokana na unafuu wa gharama zake kwa vile mtumaji
anapaswa kuwa na mtandao wa mawasiliano ya internet ambao utamuwezesha
kutuma fedha kwa haraka na kufika mara moja.
“
Jambo la kufurahisha ni kwamba kupitia huduma hizi za PBZ tunaweza
kupata Taarifa kuhusu fedha ambazo zinatumwa kuja nyumbani kutoka kwa
wenzetu walioko nje ya nchi ambazo pia zinaweza kutumiwa katika maeneo
tofauti ikiwemo Bajeti ya Serikali na Mipango ya Maendeleo “. Alifafanua
Balozi Seif.
Aliwasisitiza
wananchi walioko nje ya Nchi { Diaspora } kuendelea kutuma fedha
nyumbani kwa kupitia mtandao huo wa kusafirisha fedha kwa haraka jambo
ambalo litakuwa chachu ya kusaidia kukuza Maendeleo ya Zanzibar na
Tanzania kwa ujumla.
Mapema
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Watu wa Zanzibar Limited Nd. Juma Amour
Mohammed alisema takwimu zilizotolewa na Benki ya Dunia zimeeleza
kwamba mfumo huu wa kusafirisha fedha kutoka ughaibuni kwenda kwa jamaa
na ndugu kwenye mataifa yanayoendelea imeshafikia Dola za Kimarekani
Bilioni mia 401.
Nd.
Juma Amour aliyataja Mataifa yaliyofaidika na mfumo huo kuwa ni India,
China, Phillipines, Mexico ambapo kwa Bara la Afrika Nigeria inaongoza
kwa kupokea Dola za Kimarekani Bilioni 2.05 sawa na asilimia 9% ya pato
lake wakati Kenya kwa Ukanda wa Afrika Mashariki imepokea Dola Bilioni
1.2 sawa na asilimia 3% ya pato lake.
Mkurugenzi
Mtendaji huyo wa PBZ amewaomba Wazanzibar na Watanzania walioko
ughaibuni kuitumia fursa hiyo yenye gharama nafuu kwa kuwatumia fedha
jamaa na ndugu zao badala ya ule utaratibu wanaoutumia ambao hauko
rasmi.
Alisema
Benki ya Watu wa Zanzibar hivi sasa imefikiwa kiwango cha amana cha
asilimia 40% ikishikilia nafasi ya asilimia 16% ya mabenki yaliyomo
ndani ya kanda ya Afrika mashariki.
Alieleza
kwamba katika kuimarisha huduma za Kibenki Uongozi wa Benki hiyo tayari
imeshafungua huduma za ATM 17 ikielekea zaidi katika mtandao wa
internet na Simu.
Benki
ya Watu wa Zanzibar Limited imeshafungua matawi tisa pamoja na Matatu
yanayotoa huduma za Kiislamu hapa Zanzibar na baadhi ya Mikoa ya
Tanzania Bara tokea kuasisiwa kwake na Rais wa kwanza wa
Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume Tarehe 30 Juni mwaka 1966
Post a Comment