*************
Na Mwandishi Wetu
MKUU
wa wilaya ya Ilala Raymond Mushi amewasisitiza wadau mbali mbali
kuwekeza katika mpira wa miguu kwani hutoa ajira nyingi kwa vijana na
kuwafanya wajipatie kipato.
Akiongea
na waandishi wa habari baada ya kufunga mashindano ya Bonnah Cup
yaliyoandaliwa na diwani wa kata ya Kipawa Bonnah Kaluwa, Mkuu wa wilaya
alisema kuwa kwa miaka ya sasa mpira umekuwa kimbilo kubwa la ajira kwa
vijana kwani huweza kuwasaidia kujiingizia kipato.
Mushi
alisema kuwa pamoja na wadau kuwekeza katika mpira wa miguu, Tanzania
itaweza vile vile kukuza vipaji ambavyo huwa vinapotea.
“Tanzania
tuna vipaji vingi sana vya mpira wa miguu, tatizo ni vipaji hivyo
kuvumbuliwa hivyo nawaombeni wadau mbali mbali kutoka sekta zote
kujitokeza kuweza kuwekeza katika tasnia hii, ambapo tutawezesha vijana
wetu kujipatia ajira,” alisema.
Timu
ya Stakishari kutoka Mogo iliifunga timu ya Vipaji Halisi kutoka eneo
la airport katika fainili na kukabidiwa kombe pamoja na kiasi cha
shilingi laki tano, ambapo mshindi wa pili alipata kiasi cha shilingi
laki tatu na mpira moja na mshindi wa tatu alipata shilingi laki moja na
mpia.
Jumla ya timu 20 kutoka katika kata ya kipawa zilishiriki katika mashindano hayo.
Muandaaji
wa mashindano hayo diwani wa kata ya Kipawa Bonnah Kaluwa alisema
“Lengo kubwa ya kuandaa mashindano haya ni kuwaleta vijana pamoja
iliwaweze kufahamiana na kushirikiana lakini pia kuinua vipaji vya
vijana katika mchezo wa mpira wa miguu.
Vijana
wengi wanaocheze katika ligi hapa nchini wamechipukia katika kata ya
Kipawa. “ Napenda kuendeleza na kukuza vipaji wa vijana iliwaweze
kufikia kiwango cha juu zaidi katika mchezo huu”, alisema
Said
Mkuwa, Mwenyekiti wa mashindano hayo aliongezea: “Tunamshukuru sana
diwani kuandaa mashindano haya kwa ajili ya vijana, alisema “Nimefurahi
kwamba mashindano yamekwenda vizuri tangu mechi za mwanzo hadi fainali
na vijana wameshirikiana vizuri katika michezo yote”
CREDITS: FATHER KIDEVU BLOG
Post a Comment