Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa
Rais, Mheshimiwa Charles Kitwanga akiangalia sehemu ya kuni/magogo yaliyokusanywa
na kiwanda cha 21st Century Textile Mill mkoani Morogoro. Wengine ni Mkuu wa
Mkoa wa Morogoro Bw. Joel Bendera na Mkuu wa Wilaya Morogoro Bw. Said Amanzi
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa
Rais, Mheshimiwa Charles Kitwanga (kulia) akitoa maelezo ya kiutendaji kwa Bw.
P.V.Singh, Afisa Mtendaji Mkuu wa Kiwanda cha Century Textile Mill mkoani Morogoro juu ya
uharibifu mkubwa wa mazingira unaotokana na nishati ya kuni/magogo yanayotumiwa
kiwandani hapo katika shughuli za uzalishaji. Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa
Morogoro Bw. Joel Bendera na Mkururenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na
Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Eng. Bonaventure Baya.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa
Rais, Mheshimiwa Charles Kitwanga akikagua mfumo wa maji taka katika kiwanda
cha 21st Century Textile Mill mkoani Morogoro
*****
Na Lulu Mussa, Ofisi ya Makamu wa Rais-Mazingira
Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais,
Mheshimiwa Charles Kitwanga, hii leo amefanya ziara katika baadhi ya viwanda
Mkoani Morogoro kujionea hali ya Mazingira ikiwa ni pamoja na kuangalia mfumo
wa maji taka katika viwanda hivyo.
Katika ziara hiyo Naibu waziri Waziri ameagiza
wamiliki wa Kiwanda cha 21st Century Textile Mill kuacha teknolojia ya sasa
ambayo inatumia nishati ya miti kwa wingi.
Mheshimiwa Kitwanga ametoa agizo kwa Baraza la Taifa
na Hifadhi ya Mazingira (NEMC) kukaa na uongozi wa Kiwanda hicho kukubaliana
kimsingi matumizi ya teknolojia mbadala ya undeshaji wa shughuli za uzalishaji
katika kiwanda hicho mfano mafuta mazito, gesi na makaa ya mawe.
Sambamba na hilo Waziri Kitwanga amewataka
wamiliki wa Kiwanda hicho kutekeleza mara moja makubaliano baina yao na NEMC
juu hatua za haraka za kudhibiti uharibifu wa mazingira kwa kutumia miti mingi
katika uzalishaji wa kila siku katika kiwanda hicho vinginevyo hatua kali
zitachukuliwa ikiwa ni pamoja na kukifungia kiwanda hicho kuendelea na shughuli
za uzalishaji.
Aidha, kiwanda cha 21st Centuy pia kimepewa muda
wa mwezi mmoja kukamilisha taratibu za ukaguzi wa Mazingira (Environmental Audit) kwa kushirikiana
na Baraza la Taifa la Hifadhi ya Mazingira.
Katika hatua nyingine Mkuu wa Mkoa wa Morogoro
Mheshimiwa Joel Bendera aliyeambatana na Mheshimiwa Kitwanga katika ziara hiyo
ameagiza kusitishwa mara moja uingizwaji wa magogo katika kiwanda hicho na
kuahidi kusimamia kikamilifu zoezi hilo.
Bw. P.V. Singh, Afisa Mtendaji Mkuu wa Kiwanda
hicho ameoimba Serikali kumpa muda wa mwaka mmoja ili aweze kubadilisha mfumo
mzima wa uzalishaji unaotumia takriban tani Hamsini za kuni/magogo kwa siku.
Katika ziara ya leo Mheshimiwa Kitwanga
ametembelea Kiwanda cha Ngozi, Kiwanda cha Maturubai na Kiwanda cha Nguo 21st
Century vyote vya Mkoani Morogoro.
Post a Comment