POLISI wametambua mwili wa mwanafunzi wa
Howard University aliyeuawa kwenye jaribio la uhalifu Alhamisi
usiku. Omar Sykes, 22, na mwanafunzi mwenzake walikuwa wanatembea
maeneo ya 700 block of Fairmont Street NW kabla ya saa 5.30 usiku
walipofuatwa na watu wawili.
Polisi wanaamini kulikuwa na jaribio la
uhalifu ila yalitokea mabishano kabla mmoja ya wale watu kutoa
bastola na kumuua Sykes. Alifikia mauti kwenye hospitali ya maeneo ya
jirani.
“Tunadhani ilikuwa jambo la ghafla na
hatuna uhakika kama wanafunzi hao waliibiwa mali yoyote” alisema
Kapteni Bob Alder wa kituo cha polisi DC alipohojiwa na
News4. Mwanafunzi mwingine alipigwa na kitako cha bastola na kujeruhiwa
kichwani ingawa hana majeraha makubwa.
“Wanafunzi wengi wamepatwa na hofu ya kutoka
na kutembea usiku kwani hali hii inaogopesha sana,” alisema
mwanafunzi mmoja alipohojiwa na Megan McGrath kutoka News4.
Maelezo kamili kuhusu watuhumiwa bado
hayajapatikana. Kulikuwa na matukio mengi ya kujumuisha watu wakati wa
tukio hivyo polisi wanatumaini kuwa haitawia vigumu kwa wahalifu hao
kujulikana. Sykes alipenda uandishi na mara ya mwisho
aliandika makala kwenye mtandao unaoitwa Our Black Pages mnamo
tarehe 11 Juni. Wasifa wake unaonesha kwamba alikuwa anasomea Marketing
na Public Relations. Mkesha wa sala kwa ajili ya marehemu utafanyika
shuleni kwao Jumamosi kuanzia saa 1 usiku.
Howard University imetoa maelezo
yafuatayo kuhusiana na kifo cha Alhamisi:
“Tuna huzuni kubwa kufuatia kifo cha mmoja wa
wanafunzi wetu kilichotokea nje ya shule. Mwanafunzi mwingine alijeruhiwa
kwenye tukio hilo na anaendelea na matibabu…. Polisi wa Howard University
wanashirikiana polisi wa mji ili kupeleleza tukio hili hatari. Tunawapa pole
familia, shule na wale wote walioguswa na tukio hili kwa namna moja au
nyingine. Huduma ya ushauri nasaha itapatikana masaa 24 kwa wanafunzi wote
watakaohitaji msaada katika kipindi hiki kigumu.
SOURCE:Jestina-George.com
Post a Comment