Na Abdulaziz Video,Lindi
Halmashauri ya wilaya ya Lindi imesitisha mikataba ya ujenzi wa
barabara kwa makampuni matatu yaliyopewa tenda za kujenga barabara zenye jumla ya urefu wa km 65.2 kwa kipindi cha kuanzia mwaka 2011/13.
Hayo yamebainishwa na mhandisi wa ujenzi, Halmashauri ya wilaya
Lindi, Aswile Mwasaga alipokuwa akizungumza na timu ya waandishi wa habari waliotembelea ofisini kwake kufutia kikao cha baraza la
madiwani kulalamikia utendaji mbovu wa kazi kwa baadhi ya wakandarasi wanaopewa tenda za Ujenzi katika halmashauri hiyo.
Mwasaga alisema kuwa halmashauri imesitisha mikataba hiyo kwa baadhi ya wakandarasi kwa sababu ya utendaji wao mbovu na kutozingatia muda wa kazi na kusababisha miradi hiyo kuchelewa kukamilika kwa wakati uliopangwa na kujengwa chini ya kiwango kilichokusudiwa
Aswile Aliyataja makapuni hayo kuwa Mwombe Company Ltd iliyopewa barabara za Rutamba ,Mnara,Nyengedi,17.7Milola Kiwawa km12,na Steven Roadwork barabara ya mipingo,Mnyangara,km 8.5, na Mkwajuni, Namkongo Km 19. Alisema kampuni nyingine ni Montanga Constraction iliyopewa kazi katika barabara ya Nachunyu,Mmumbu yenye km 8.
Aidha Aliongeza kuwa kuna makampuni mawili ambayo Bhavik
constraction na Macroteck yamechelewesha kazi na kupewa adhabu ya kusimashwa kwa muda
Kufuatia hali hiyo tuliwasiliana na mkurugenzi wa kampuni ya Bhavik
Constraction Hitesh Mehta ambae alisema kuwa alisimamisha kazi hiyo
kutokana na mvua nyingi zilizokuwa zinanyesha hapo awali lakini
baada ya mvua kukatika kazi inaendelea na utekelezaji wake umefikia
asilimia 90 ya kazi aliyopewa na kwa kiwango bora kwa mujibu wa
mkataba
Via Lindi Yetu
Post a Comment