Peter
Kang (kulia) akiwa na mmoja wa akitembelea baadhi ya kaya zilizopewa
machujio ya kutibu maji eneo la Kiwalani, jijini Dar es Salaam.
Peter
Kang (kulia) akiwaonesha wananchi maji ambayo yamefanyiwa utafiti na
kujulikana yapo salama baada ya kuchujwa na machujio hayo
Baadhi ya wananchi wakielimishwa juu ya teknolojia hiyo leo
BAADHI
ya familia eneo la Kiwalani jijini Dar es Salaam zimenufaika na
teknolojia ya kutibu maji kirahisi na kuwa safi na salama kwa matumizi
ya nyumbani. Timu ya wanachuo watafiti kutoka nchini Korea inayojulikana
kwa jina la AQUA ndiyo inayoratibu programu hiyo ya majaribio ya
kuwezesha kaya kupata maji safi na salama kwa matumizi.
Programu
hiyo inayotarajia kuenezwa maeneo mbalimbali nchini Tanzania imeanza
kwa kuzipatia kaya 15 machujio rahisi yaliotengenezwa kuchuja maji na
kuyatibu ili yawe safi na salama kwa matumizi ya binadamu moja kwa moja.
Akizungumza
kiongozi wa jopo hilo la wanachuo (AQUA), Peter Kang alisema utafiti
wao umefadhiliwa na Massachusetts Institute of Technology chini ya
usimamizi wa Profesa Hong Seong hapo baadaye programu walioanzisha
itasambazwa maeneo anuai ya Tanzania.
Alisema
programu hiyo mbali ya kusaidia familia kupata maji safi na salama
itawaondolea wanawake kero ya kusaka maji safi na salama kundi ambalo
ndilo lenye majukumu ya kutafuta maji kwa ajili ya matumizi ya familia
nyumbani.
Aidha
alisema programu hiyo imeonekana kupokelewa kwa muitikio mzuri huku
wanawake wakiwa mstari wa mbele kwani baadhi ya vikundi vimekuwa
vikijipatia kipato kwa kuziuzia familia kadhaa maji hayo safi na salama
baada ya kutibiwa. Alisema hata hivyo programu hiyo imepokelewa kwa
muitikio mzuri haswa na akinamama ambao kikawaida katika kaya nyingi
hutimia muda mrefu kufuatilia maji kwa ajili ya matumizi ya nyumbani.
Kwa
sasa AQUA wametoa jumla ya machujio 15 yenye ujazo wa lita 60 kwa
majaribio kwa baadhi ya kaya na kaya hizo zitatakiwa kuchangia kiasi cha
shilingi elfu 5,000 kwa mwezi na baadaye watakabidhiwa umiliki wa
machujio hayo moja kwa moja. Machujio hayo yanauwezo wa kuchuja na pia
kuuwa wadudu hatari kwa afya ya binadamu kwenye maji na kuyaacha maji
safi na salama kwa matumizi.
Naye
Mratibu wa Mafunzo na Maendeleo, Denis Mnyanye kutoka 'Son
International' ambao ni watengenezaji wa machujio hayo alisema
teknolojia hiyo ni rahisi na salama hivyo kuomba jamii kuiunga mkono,
hasa ukizingatia kiasi kikubwa cha maji yanayotumika baadhi ya maeneo
nchini si salama kutokana na mazingira yetu.
"...kutokana
na mfumo wetu wa usambazaji maji na miundombinu yake kuna uwezekano
baadhi ya maeneo watu wakapokea maji ambayo si salama, au yale
yanayopatikana baadhi ya fisima lakini ukitumia machujio haya nyumbani
unayatibu maji yako mwenyewe hivyo kuwa salama zaidi," alisema Mnyanye.
Post a Comment