|
Waziri Mkuu mstaafu Mhe. Edward Lowassa akizungumza na
wananchi waliojitokeza katika hafla ya Harambee iliyofanyika katika Hotel Gold
Crest jijini Mwanza, kuwahamasisha kutambua nini wanapaswa kufanya ili
kufanikisha lengo lililokusudiwa. |
Na Albert G.
Sengo
MWANZA.
WAZIRI Mkuu mstaafa
Mhe.Edward Lowassa ijumaa usiku aliongoza harambee kubwa na ya kihistoria ya
kuchangia kituo cha Redio IQRA Fm kinachomilikiwa na Baraza Kuu la Waislamu Mkoa
wa Mwanza (BAKWATA) iliyofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Gold Crest Jijini
Mwanza.
Mhe.Lowassa aliyekuwa Jijini Mwanza kushirikiana na
marafiki zake, wafanyabiashara, taasisi na makampuni mbalimbali, watu binafisi
na viongozi wa serikali na vyama vya siasa na wabunge wa majimbo mawili ya
jijini Mwanza Ilemela na Nyamagana kupitia CHADEMA yaliyotuma wawakilishi wao
hatimaye aliweza kuvuka lengo lililowekwa kwa kukusanya zaidi ya shilingi
milioni 590 zikiwemo ahadi.
|
Mfanyabiashara maarufu jijini Mwanza ambaye pia ni Mzee
wa baraza la wazee Mwanza Mjumbe wa NEC wilaya ya Tarime Mhe. Christopher
Gachuma akimkabidhi mmoja wa wazee wa kiislamu aliyeketimeza kuu kanzu pamoja na
joho kama zawadi aliyovikwa mgeni rasmi Mhe.
Lowassa. |
|
Lilikuwa tukio la kipekee Mhe. Lowassa alivikwa na
kukabidhiwa zawadi ya kibarakashia
juu.. |
"Ninaamini vituo vya redio
Iqra FM na redio Sauti ya Qur-ani kitaonyesha Uislamu kama dira unayohusisha
mambo yahusuyo jamii. Ni cheche ya kimungu ambayo inatoa ubinafsi pia inayo
waunganisha binadamu katika jamii moja. Korani inasema binadamu ameumbwa
kutokana na roho moja, kama mwanaume na mwanamke, jamii na mataifa, ili watu
waweze kufahamiana. Inawaleta watu wa imani zote kwenye jukwaa moja, kwa kupitia
wema."
CHANGIZO
LIKAANZA:
Post a Comment