Mkuu wa JKT
Meja Jenerali Raphael Muhunga akitoa hotuba yake wakati wa uzinduzi wa michezo
ya kusherehekea miaka 50 ya JKT iliyoanza leo katika viwanja vya Kumbukumbu ya
Karume jijini Dar es Salaam. (Picha na Habari Mseto Blog)
Baadhi ya
wachezaji wakipita kwa maandamano mbele ya mgeni rasmi wakati wa uzinduzi wa
michezo ya kusherehekea miaka 50 ya JKT.
Macho
mbeleee.
Mkuu wa
JKT Meja Jenerali Raphael Muhunga akisalimiana na wachezaji wa timu
ya Kanembwa
JKT ya Kigoma.
Mkuu wa
JKT Meja Jenerali Raphael Muhunga akisalimiana na wachezaji wa JKT Ruvu kabla ya
mpambano wao na Kanembwa JKT.
Mgeni
rasmi akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa timu zote mbili.
Na
Elizabeth John
JESHI la
Kujenga Taifa (JKT), limezindua michezo mbalimbali kuelekea maadhimisho ya
kusherehekea miaka 50 tangu kuanzishwa kwake.
Michezo
hiyo imezinduliwa leo katika uwanja wa Karume na maadhimisho yake yatafanyika
Julai 10 katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Akizungumza
wakati wa uzinduzi huo, Meja Jenerali Raphael Muhunga ambaye ndio alikua mgeni
rasmi katika uzinduzi huo aliwataka wanamichezo kufanya vizuri katika mashindano
hayo ambapo kutakua na zawadi kwa washindi siku ya kilele cha maadhimisho
hayo.
Alisema
lengo la mashindano hayo ni kuadhimisha miaka 50 ya JKT ambayo yataenda sambamba
na maonesho mbalimbali ambayo pia yatazinduliwa rasmi leo katika kikosi cha 831
Mgulani JKT.
Alisema
timu nne za JKT ambazo zinashiriki ligi kuu Tanzania Bara, Ruvu Shooting, Mgambo
Shooting, JKT Oljoro na JKT Ruvu zitakua zinaiwakilisha JKT ikiwa ni pamoja na
timu ambazo zinacheza ligi daraja la kwanza Tanzania bara, Kanembwa JKT ya
Kigoma na Mlale JKT ya Ruvuma.
“Tunategemea
kwa hapo baadae, JKT kupitia kurugenzi ya Elimu na Michezo inatakiwa kuwa na
shule ya kukuza vipaji vya wanamichezo kama zinavyofanya nchi za wenzetu,
tunaamini kwa kufanya hivi michezoitakua hapa nchini.
Alisema JKT
wanaendelea kuwatumia vijana wanaojiunga na mafunzo ya JKT ili kupata achezaji
bora watakaoliwakilisha Taifa letu katika michezo mbalimbali ya
Kimataifa.
Post a Comment