Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

KIKONGWE AUAWA HUKO SIKONGE TABORA

KIKONGWE aliyefahamika kwa jina la Mwalu Kulwa (70), mkazi wa kitongoji cha Maria, Wilaya ya Sikonge, mkoani Tabora, ameuawa na watu wanaosadikiwa ni majambazi kwa kukatwakatwa mapanga mwilini.

Diwani wa Kata ya Kiloleli, Boniphace Mlimakala Mtani, alisema hayo wakati akiongea na waandishi wa habari wilayani humo.

Mtani alisema kuwa tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia Jumatatu wiki hii majira ya saa 2:00 usiku nyumbani kwa marehemu Kulwa.

Diwani Mtani alisema Mwenyekiti wa Kitongoji cha Maria, Shija Luhumboka, alitoa taarifa kwa ofisa mtendaji wa Kata ya Kiloleli kwa simu saa 8:00 usiku baada ya kutokea kwa tukio hilo.

Mtani alisema watu hao walimtoa kikongwe huyo ndani ya nyumba yake na kumkata kwa panga nje ya nyumba hiyo kisha kutoweka na hadi sasa chanzo cha mauaji hayo bado hakijafahamika.

Alisema polisi walijulishwa tukio hilo na kufika eneo la tukio na kuamuru mwili wa kikongwe huyo uzikwe, huku mkuu wa polisi wa wilaya hiyo, Mwambongo akiwataka wakazi wa kijiji hicho kufufua jeshi la sungusungu ili kudhibiti hali hiyo.

SOURCE::JAIZMELALEO
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top