Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Mahakama ya Hakimu Mkazi Mjini Singida Yatupilia Mbali kesi iliyokuwa inawakabali viongozi wawili wa CHADEMA Afisa Sera na Utafiti Makao Makuu Mwita Waitara na Mshauri Wa Chadema Dk Kitila Mkumbo

Afisa Sera na Utafiti Makao Makuu  Ndugu Mwita Waitara 
--
 Mahakama ya Hakimu Mkazi Mjini Singida  jana imetupilia mbali kesi iliyokuwa inawakabali viongozi wawili wa CHADEMA Ndugu Mwita Waitara ambaye ni afisa sera na utafiti makao makuu na mshauri wa chama hicho Dk Kitila Mkumbo. Katika hukumu yake aliyeiosoma mbele ya wakili wa washtakiwa hao Tundu Lissu Hakimu wa Mahakama hiyo Masham alisema kuwa washatakiwa hawana kesi ya kujibu kwa kuwa mashahidi wa serikali walishindwa kuthibitisha aina ya matusi yaliyodaiwa kutolewa na washtakiwa.
 Aidha, hakimu huyo alisema kwamba upande wa serikali walishindwa kumleta shahidi muhimu katika kesi hiyo Mwigulu Nchemba aliyedaiwa kutukanwa ili athibitishe kwamba yeye ndiye aliyetukanwa na namna ambavyo matusi hayo yamemuathiri. Kushindwa kwa Mwigulu Nchemba kufika mahakamani ni kuonyesha kwamba ama hajui kwamba alitukanwa au hakuona kosa lolote alilotendewa na mahakama haiwezi kutoa uamuzi kwa mambo ya kuhisiwa, alisema hakimu huyo. 

Washtakiwa walidaiwa kutenda kosa hilo tarehe 14 Julai mwaka jana katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Ndago wilayani Iramba ambapo Chama cha Demokrasia na Maendeleo kilikuwa na mkutano wa hadhara. Kesi hiyo imekuwa ikisuasua mara nyingi kwa upande wa serikali kushindwa kuleta mashahidi mahakamani na kusababisha kesi hiyo kuahirishwa mara kwa mara, jambo ambalo lilikuwa likimkera hakimu wa kesi hiyo.

Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top