Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibarf Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na
Wajumbe wa Kamati ya Wafanyabiashara ya kushajiisha ushiriki wa Sekta
Binafsi katika maadhimisho ya Sherehe za kutimia miaka 50 ya
Zanzibar aliokutana nao Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar. Picha na Hassan Issa-Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar
---
Wazanzibari
wote walioko ndani na nje ya Zanzibar wana fursa, haki na Uhuru wakati
wowote kusaidia kwa njia mbali mbali maandalizi na hatimae kufanikisha
sherehe za Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964 kutimia robo Karne ambayo
ni sawa na miaka 50 iliyopita.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema hayo wakati
akizungumza na Wajumbe wa Kamati ya Wafanyabiashara ya kushajiisha
ushiriki wa Sekta Binafsi katika maadhimisho ya Sherehe za kutimia miaka
50 ya Zanzibar aliokutana nao hapo Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.
Balozi
Seif alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imelenga kuwaungalisha
Wazanzibari wote popote pale walipo ili kuona wanashiriki kikamilifu
kwenye maadhimisho hayo yanayotarajiwa kuwa ya aina yake na Kihistoria
hapo mwakani.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliieleza Kamati hiyo baadhi ya mambo
yaliyopangwa kufanya ndani ya vugu vugu la maadhimisho hayo ambayo
yatasaidia kutoa taaluma kwa Jamii hasa kile kizazi kilichozaliwa baada
ya mapinduzi ya mwaka 1964 ambacho bado hakijaelewa dhamira hasa ya
kufanyika kwa Mapinduzi ya Zanzibar.
Balozi
Seif ambae pia ni Mwenyekiti wa Sherehe na Maadhimisho ya Taifa
aliyataja baadhi ya mambo yaliyolengwa kufanya katika kipindi hicho cha
sherehe kuwa ni pamoja na warsha, makongamano kwa kushirikisha vyama vya
Siasa, matembezi ya kuashiria sherehe hizo pamoja na usiku maalum wa
burdani na ngoma za asili.
Alifahamisha
kwamba Mnara Maalum wa kumbu kumbu ya Mapinduzi utajengwa ili kupamba
sherehe hizo za aina yake zitakazotoa pia fursa ya kualikwa kwa Viongozi
wa nchi rafiki za mwanzo zilizojitokeza kuunga mkono mapinduzi ya mwaka
1964.
“
Katika kupamba sherehe zetu tumeandaa kutoa nishani maalum kwa watu
waliotoa mchango mkubwa kwa Taifa tokea Mapinduzi ya Mwaka 64 wakiwemo
askari wa Vikosi vya ulinzi na usalama, wana sanaa na Utamaduni “.
Alisisitiza Mwenyekiti huyo wa Kamati ya sherehe na maadhimisho ya
Taifa.
Balozi
Seif aliwaomba wajumbe wa Kamati hiyo ya Wafanyabiashara ya kushajiisha
ushiriki wa Sekta Binafsi katika maadhimisho ya Sherehe za kutimia
miaka 50 ya Zanzibar kuhakikisha wanajitolea kwa nguvu zao zote katika
kufanikisha vyema kazi waliyopewa na Taifa.
Naye
mjumbe wa Kamati hiyo Mbunge wa Jimbo la Mpendae Salum Turky aliahidi
akujitolea kugharamia ujenzi wa mnara huo wa kumbu kumbu ya Mapinduzi
unaotarajiwa kujengwa katika eneo la Mzunguuko wa Bara bara za makutano
ya Nyumba za Maendeleo Michezani.
Aliiomba
Kamati ya Sekriterieti ya Sherehe na Maadhimisho ya Taifa Zanzibar
kumpatia michoro ya ujenzi wa Mnara huo ili apate wasaa wakujiandaa
kuitekeleza kazi hiyo ambayo anaamini kwamba atakuwa ametoa mchango na
kuweka historia ndani ya maadhimisho ya sherehe za Mapinduzi ya
Zanzibar.
“
Tunashukuru kuona kwamba Zanzibar inaingia kutimiza miaka hamsini ya
Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964 ikiwa katika hali ya amani na
utulivu hali ambayo ni nadra kupatikana katika baadhi ya Nchi Duniani “.
Alifafanua Mjumbe huyo wa Kamati hiyo Salum Turky.
Kwa
upande wao wajumbe wengine Simai Mohd, Ahmada Abdullwakil, Sharifa
Khamis na Meneja wa Kampuni ya Simu za Mkononi ya Zantel Zanzibar
Mkweche wameipongeza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa uamuzi wake
wa kuanza kujiandaa mapema ya sherehe hizo kubwa.
Hata
hivyo waliishauri Serikali kufikiria kutenga maeneo ambayo
wafanyabiashara wanaweza kuyatumia kutangaza biashara zao katika njia
maalum itakayotoa fursa ya kuchangia maadhimisho hayo.
“
Sio mbaya kwa Serikali kutafuta njia ya kuwashirikisha pia
Wafanyabiashara wa Tanzania Bara hasa wale waliowekeza vitega uchumi
vyao hapa Zanzibar na pia wenye imani ya muelekeo wa kuunga mkono
maadhimisho hayo “. Alisisitiza Simai Mohd.
“
Wakati tumejikubalisha na sisi kuingia katika ulimwengu wa sayansi na
tenolojia na kwa vile wenzetu wamejiimarisha vyema katika masuala ya
utambulisho wao itapendeza nasisi kuelekea huko kwa kuwa na utambulisho
wetu maalum ambao utawapa fursa wageni na watalii kuielewa vyema
Zanzibar“. Alishauri pia Mjumbe mwengine wa kamati hiyo Ahmada Abdull
wakil.
Katika
kuanza rasmi jukumu zima walilopewa wana kamati hao walifikia
uwamuzi wa kuanza kikao cha dharura mara baada ya mkutano huo kupanga
mikakati ya kufanikisha jukumu lao.
Ujumbe
wa mwaka huu wa Maadhimisho ya sherehe za Mapinduzi ya Zanzibar kutimia
robo Karne { sawa na miaka 50 } ni Amani, Umoja na Maendeleo yetu ni
Matunda ya Mapinduzi ya 1964. “ Mapinduzi Daima “.
Post a Comment