Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa, akipongezwa na kiongozi wa Sunni al Jamaa Afrika Mashariki, Shariff Hussein al Badawi kwa kumvika joho la kilemba baada ya kufanikisha harambee kwa ajili ya Kituo cha Redio Ikra kinachomilikiwa na Baraza la Waislamu Tanzania (Bakwata) Mkoa wa Mwanza.
Anayeshuhudia ni Sheikh wa Mkoa wa Mwanza, Sheikh Salum Hassan Fereji.
Katika harambee hiyo zaidi ya sh. mil. 590 zilipatikana na kuvuka lengo ambalo lilikuwa sh. mil 500.
WAZIRI Mkuu mstaafu Mhe.Edward Lowassa ijumaa usiku
aliongoza harambee kubwa na ya kihistoria ya kuchangia kituo cha Redio IQRA Fm
kinachomilikiwa na Baraza Kuu la Waislamu Mkoa wa Mwanza (BAKWATA) iliyofanyika
katika ukumbi wa Hoteli ya Gold Crest Jijini Mwanza.
Mhe.Lowassa aliyekuwa Jijini Mwanza kushirikiana na marafiki zake, wafanyabiashara, taasisi na makampuni mbalimbali, watu binafisi na viongozi wa serikali na vyama vya siasa na wabunge wa majimbo mawili ya jijini Mwanza Ilemela na Nyamagana kupitia CHADEMA yaliyotuma wawakilishi wao hatimaye aliweza kuvuka lengo lililowekwa kwa kukusanya zaidi ya shilingi milioni 590 zikiwemo ahadi.
Post a Comment