Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

MIRADI MIKUBWA YA UMEME, VIGOGO WAAPISHWA KUJIUZULU WAKISHINDWA.

 

Miundombinu ya umeme iliyopo kwa sasa nchini.
Serikali imeweka wazi miradi ya umeme ya kipaumbele, itakayotoa matokeo ya haraka ifikapo 2015/2016, na kunufaisha wananchi katika mikoa 13 nchini.
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, alisema hayo jana mbele ya wadau waliokusanyika katika mkutano wa siku moja wa kukusanya maoni kuhusu utekelezaji wa miradi hiyo.

Alisema wizara hiyo imedhamiria kuhakikisha miradi
hiyo kwa kipindi hicho, inaleta matok
eo muafaka yatakayoonekana wazi kwa Watanzania wote.
Aliitaja miradi hiyo kuwa ni pamoja na bomba la gesi kutoka Mnazibay hadi Dar es Salaam, lenye urefu wa Kilometa 534, ambalo litagharimu dola za Marekani bilioni 1.2. 
ÒNasisitiza acheni malumbano ya kipuuzi na malalamiko yasiyo na tiba, bomba hili lazima likamilike ndani ya miezi 18,Ó alisema Muhongo.
Alisema wote wanaopinga kutandikwa kwa bomba hilo, hawaitakii mema Tanzania na wananchi wake na kwamba hoja zao zimejaa ubaguzi.
ÒNaomba tusipoteze muda kujadili bomba hili, wapo watu wana sababu zao, hii gesi itanufaisha Watanzania wote wakiwemo wa Mtwara, tusikubali ujinga wa mtu mmoja uwe wa taifa zima,Ó alisisitiza.
Alitaja miradi mingine kuwa ni mitambo saba mipya ya Kinyerezi, itakayozalisha megawati za umeme 1,310, itakayozalisha megawati 990, na mradi wa upepo wa Singida wa megawati 50 na Kiwira wa megawati 200.
Miradi mingine ni ya ujenzi wa njia za usambazaji umeme, ambazo ni Iringa-Shinyanga yenye kilometa 657 utakaosambaza umeme wa KV 400 na Dar es Salaam-Chalinze-Tanga-Same-Arusha, wenye kilometa 682 utakaosambaza umeme wa KV 400.
CREDIT ZIRRO
Pia upo mradi wa Singida-Arusha wa kilometa 414 utakaosambaza umeme wa KV 400, Somanga-Fungu-Somanga-Kinyerezi wa kilometa 300, utakaosambaza umeme wa KV 220.
Mradi mwingine ni wa Nyakanazi-Kigoma-Mpanda-Sumbawanga-Mbeya, wenye kilometa 340 utakaosambaza umeme wa KV 400 na Dar es Salaam-Morogoro-Dodoma wenye urefu wa kilometa 530, utakaosambaza umeme wa KV 400.
Ili kuhakikisha kila mradi, utekelezaji unasimamiwa vilivyo, wakurugenzi wanne walioko chini ya Wizara ya Nishati na Madini, watakaowajibika kutekeleza miradi hiyo, wameapa mbele ya wananchi kuwa watafanikisha matokeo ya miradi hiyo, vinginevyo wako tayari kutimuliwa kazi.
Wakurugenzi hao ni pamoja na Mkurugenzi wa Shirika la Umeme (Tanesco), Felchesmi Mramba na  Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC), Yona Killagane.
Wengine ni Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Usambazaji Umeme Vijijini (REA), Lutengano Mwakahesya pamoja na Kamishna wa Nishati na Petroli, Hosea Mbise ambaye ndiye msimamizi mkuu wa miradi hiyo.
Wakurugenzi hao walitoa kiapo hicho mbele ya wadau waliokusanyika katika mkutano wa siku moja ulioandaliwa na wizara hiyo, kwa ajili ya kukusanya maoni juu ya utekelezaji wa miradi hiyo yenye matokeo makubwa nchini ifikapo mwaka 2015/2016.
Akizungumza mara baada ya kuapa mbele ya wadau hao, Mbise, alisema wizara hiyo imedhamiria kuhakikisha kuwa miradi hiyo kwa muda huo, inaleta matokeo muafaka yatakayoonekana wazi kwa Watanzania wote.
ÒNi kweli kumekuwepo na miradi mingi ya wizara hii kwa muda mrefu, lakini sasa nawaahidi kuwa tunakuja na njia mpya ya kuzingatia miradi michache, lakini matokeo yake pamoja na kuonekana haraka, yatanufaisha Watanzania wengi.
ÒNinawaahidi katika utekelezaji wa miradi hii, tutaachana kabisa na tabia ya kufanya kazi kwa mazoea,Ó alisisitiza.
Kwa upande wake Mramba, alisema miradi hiyo, sehemu kubwa itatekelezwa na shirika lake. 
Nawaahidi Tanesco haitowaangusha, ninaamini uwezo wa kuleta matokeo haya makubwa ninao, nikishindwa niko radhi mnichukulie hatua.
ÊKillagane naye alisema ili kufanikisha miradi yote hiyo, jambo la msingi ni kuhakikisha gesi inapatikana kwa haraka, ambapo kwa mujibu wa maelekezo ya TPDC, ni lazima bomba la gesi kutoka Mnazibay mkoani Mtwara hadi Dar es Salaam, liwe limetandikwa na kukamilika ifikapo Juni mwakani.
ÒHili nitasimamia kwa dhati kuhakikisha gesi hii inafika jijini hapa mwakani kama ilivyopangwa, TPDC tumejipanga ili kuhakikisha hii kazi haikwami,Ó alisisitiza.
Mwakahesya ambaye ni Mkurugenzi wa REA, alisema jukumu lake katika utekelezaji wa miradi hiyo, ni kushirikiana na sekta binafsi na ya umma, ili umeme ufike vijijini. ÒSi maneno bali ni vitendo, niwajibisheni kama sitafanikisha haya.
Muhongo alisema anaamini watendaji hao hawawezi kumdanganya yeye wala Watanzania, kwa kuwa anao uzoefu wa kutosha kubaini iwapo anadanganywa.
ÒNaomba mkiona mtu anafanya kazi chini ya wizara yangu hii kinyume na taratibu, mleteni kwangu na nina ahidi mbele ya wananchi hawa kuwa sababu zitakazomuondoa mtumishi wa wizara hii kazini, ni pamoja na rushwa, wizi, utendaji mbovu na ubababishaji, hapa hakutakuwa na mjadala, nyie mtaona tu watu wakipukutika,Ó alisisitiza.
Kuhusu umeme vijijini, Muhongo alisema kupitia mpango wao walioainisha wa umeme vijijini, watahakikisha kila mwaka kwenye kila mkoa, vijiji kadhaa vitakavyobainishwa kulingana na idadi ya watu wake, vitapatiwa umeme na tayari Sh bilioni 330 zimetengwa kwa ajili ya kazi hiyo.
Alisema miradi hiyo ikikamilika, Tanzania itakuwa inazalisha megawati za umeme 2,780 na lengo ni kuhakikisha ifikapo mwaka 2025, megawati za umeme 3,000 zinazalishwa na asilimia 56 ya Watanzania wana umeme. Kwa sasa megawati za umeme zinazozalishwa ni 1,430.24 wakati mahitaji ni megawati 850.
Ili kufanikisha malengo hayo, Muhongo alisema tayari hatua za kubomoa Tanesco zimeshaanza kuchukuliwa,  kwa sasa mchakato wa kumtafuta mshauri kwa ajili ya kufanyia kazi ripoti ya menejimenti ya shirika hilo, juu ya namna liwe, umeanza kwa ufadhili wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB).
Mapendekezo ya awali yanaonesha shirika hilo litabomolewa na kugawanywa, ambapo sehemu za uzalishaji, usambazaji na usafirishaji umeme zitajitegemea, kwa kuwa na kampuni zaidi ya tatu, ambazo hazitotegemea ruzuku ya Serikali.
Kwa upande wa TPDC, Muhongo alisema Serikali pia italifumua shirika hilo kutoka kwenye muundo wake wa sasa, na kuwa shirika kubwa litakalofanya utafiti na uvunaji wa gesi na mafuta, kama kampuni kubwa za kigeni zinavyofanya ili kuondoa malalamiko ya nishati hiyo kuibiwa na wageni.
Katika hatua nyingine, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi, alisema tayari alishafuatwa na watu kadhaa ambao walitaka kumpa rushwa, ili miradi yao mibovu itekelezwe na Serikali.
ÒKuna mtu alikuja akaniambia nikiweka saini kwenye mradi wake, atanipa dola za Marekani 200,000 ambazo ni sawa na Sh milioni 350, nikamkatalia na kumtaka aondoke haraka na mradi wake uchwara,Ó alisema.
Kuhusu kusafisha Tanesco, alisema hadi kufikia Desemba mwaka jana na Juni mwaka huu, Shirika la Umeme (Tanesco), tayari limefukuza kazi watumishi 49 wanaotuhumiwa kuhusika na rushwa na kulihujumu shirika hilo.

Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top