Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Mohamed Chande Othman akiondoka katika
Banda la Jeshi la Magereza baada ya kujionea bidhaa mbalimbali zikiwemo
samani za majumbani na bidhaa za viwandani kama inavyoonekana katika
Picha huku akiwa ameongozana na Maofisa mbalimbali aliofuatana nao
Mshauri Mwelekezi wa Mradi wa Ujenzi wa Kiwanda cha kutengeneza Kofia
Ngumu katika Gereza Kuu Ukonga, Bw. Alpherio Nchimbi akimwelezea Jaji
Mkuu wa Tanzania, Mhe Mohamed Chande Othman namna Kofia hizo zenye ubora
zinavyotengenezwa. Kiwanda cha kutengeneza Kofia ngumu kipo katika
hatua za mwisho za kukamilika na Ujenzi wake upo Gereza Kuu Ukonga, Dar
es Salaam
Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman(wa kwanza kushoto)
akiangalia meza yenye viti viwili iliyotengenezwa kwa miti ya Henzerani
inayopatikana Mkoani Kigoma, anayemwelezea Jaji Mkuu ni Kamishna
Msaidizi wa Magereza, Alexanda Mmasy.
Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman akiangalia Sofa seti
ambayo imetengenezwa na Wafungwa wa Gereza Kuu Ukonga kwa kushirikiana
na Mafundi wa Jeshi la Magereza. Anayemwelezea ni Kamishna Msaidizi wa
Magereza, Alexanda Mmasy.Picha na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza
Post a Comment