Mwarabu aliyetembea kwa Miguu Dar es salaam mpaka Tanga.
Baba yake alitembea kutoka Dar es salaam mpaka Kigoma
Yafuatayo ni mahojiano yaliyofanyika kati ya mwandishi na mzee Abdullah Mohammed Alruweihy mwaka 2007 katika kijiji cha Saadani eneo la Tongoni wakati wa uhai wake.Alifariki mwaka 2009/2010.Mwenyezi Mungu amrehemu.
Swali:Sisi pale jijini Tanga tunakufahamu zaidi kwa jina la mzee Ruwehi.Jina lako kwa ukamilifu ni nan?.
Jibu:Mimi jina langu ni Abdullah bin Muhammad bin Habiib bin Salim bin Ally bin Suleiman bin Salim Al Rawaahy.
Swali:Umezaliwa wapi?.
Jibu:Nimezaliwa kijiji cha Ndono kwa Mwana Kurwa Tabora.
Swali:Tupe historia ya wazazi wako kwa kifupi.
Jibu:Mama yangu alikuwa akiitwa Zuhura
kutoka kabila la Manyema.Baba yangu alikuwa ni mmoja ya wafanyaji wa
biashara aliyetoka kutoka nchi ya Oman.Alikuja mpaka Zanzibar.Akaona
Zanzibar hapamfai akaondoka kuelekea sehemu za bara.Akafika sehemu moja
inaitwa Tabora kama nilikutajia.
Sasa
baada ya kufika hapo.Huyu bwana alikuwa anafanza kazi za
biashara.Wakati huo walimchunuka Majarumani.Na ikawa wanatumia vitu
vingi katika dukani kwake.
Sasa ilipokuwa imetokea ile vita wak
awa majarumani wanashambuliwa na waiengereza.
Swali:Ni vita gani hiyo?
Jibu:Ni vita ya 1914
Swali:Jee ndiyo ile vita ya mwanzo ya dunia?.
Jibu:Hapana,haikuwa vita ya mwanzo ya dunia.Ile vita ya maji maji ni vita mbali ile.Hii ilikuwa ni vita ya pili.
Swali:Ilikuwa ni mwaka gani?.
Jibu:Ilikuwa ni 1914.
Swali:Wewe ulizaliwa mwaka gani hasa?.
Jibu:Mimi nilizaliwa tarehe 10/02/1908
Swali:Tuendelee na historia ya wazazi wako.
Jibu:Mzazi wangu mbali na kufanza utaratibu akawa na mlahaka na wale wajarumani mpaka ilipoingia vita.
Vita
iliendelea mpaka baadae akaja mmoja anaitwa bwana Robert Fonreto.
Akamwambia Muhammed una habari?.Vita inaendelea vikali na sisi hapa
tulipo hatukukaa vizuri.Akamwambia sasa tutafanza nini?.Akamwambia
risasi imekuwa kidogo na baruti kidogo lakini askari wapo wa kuweza kuendesha kazi.Sasa tutafanza mashauri gani?.
Akamwambia kama shauri ya risasi na baruti mimi nitafanza taratibu ya kuweza kutafuta na maarif mengine.Akamwambia unaweza kweli,akajibu ndio.Akamwambia haya ondoka nenda.
Akaondoka
moja kwa moja mpaka akafika Dar es salaam.Wakati ule wajarumani wenyewe
ndio wameikamata Dar es salaam.Akatoka Dar es salaam moja kwa moja
mpaka akafika kwenye nchi ya Mukkalla,Yemen.Akatoka Mukalla akenda
juu,akapata risasi na baruti jumla debe thamanini na nne (84).
Ikawa
chini akaweka risasi na madebe mengine akaweka baruti,lakini juu
akaweka tende.Akaajiri jahazi moja lakini mimi wakati ule bado
mdogo.Lakini ile historia walivyokuwa wananieleza wale waliiokuwa wenziwe.
Akasikilizana
na nahodha kuwa hii ni tende nipelekee Dar es salaam.Nahodha akaondoka
mpaka akafika Unguja.Wakati ule Unguja ilikuwa ndani ya mikono ya
waarabu wenyewe.Unguja ana nduguze.Mmoja anaitwa sheikh Suleiman bin
Said Alruwahiy.Anakaa sehemu moja kule Unguja panaitwa Michungwa miwili.
Walipofika
kule wakamwambia habari gani uliyonayo Mohammed?.Aliwaambia sina habari
yoyote.Nimekuja tu kuwasalimia.Hakuwaambia ile siri yake.
Ile
jahazi baada ya pale akamwambia chukua hii mizigo kateremshe Dari
salaam.Mimi nipo kidogo hapa halafu nakuja.Nahodha akaendesha jahazi
hadi Dari salaam.Wakati ule ilipofika ile jahazi Dari salaam haipo tena
ndani ya mikono ya Wajarumani.Imo ndani ya mikono ya
Muiengereza.Kashatawala muiengereza. ITAENDELEA...
CHANZO http://www.islamictides.com
Post a Comment