Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Simulizi Za Mzee Madiba; Siku Mandela Alipofika Nyumbani Kwa Nyerere Msasani...!

               


6 c516b
 
Na Maggid Mjengwa,
Tunaendelea na simulizi hizi za Mzee wetu Madiba. Nilisimulia jinsi Mandela alivyofanya safari ya hatari angani. Safari ya kutoka  Bachuana Land kuitafuta Mbeya katika ardhi ya Tanganyika. Ilikuwa ni mwaka 1962.
Kimsingi Mandela na ANC walitaka wafike Addis Ababa kwenye mkutano walioalikwa rasmi. Ni mkutano  wa PAFMESCA ambao ungeshirikisha nchi na viongozi wengi wa nchi za Afrika zilizokuwa huru wakati huo. Ilikuwa ni fursa  kwa Mandela kufungua milango ya mawasiliano na viongozi mbali mbali kwa manufaa ya ANC na mapambano yao ya ukombozi kutoka ubaguzi wa rangi.
Na kabla ya kuendelea na kuiangalia safari yake ya kwenda Dar, ebu kidogo tubaki Mbeya, tuone ni jinsi gani Mandela alivyoitafakari nchi yake ya kwanza ya Kiafrika aliyoiona tangu azaliwe. Ikumbukwe,
kwenye safari yake ya Tanganyika, Mandela aliongozana na Bw. Joe Matthews, Mzungu mwanaharakati wa kupinga ubaguzi na mwanachama wa ANC.
Mandela alishangazwa sana na aliyoyaona pale Mbeya, na hususan pale kwenye hoteli waliyofikia. Na hapa Mbeya inaingia katika historia kuwa ni mji wa kwanza wa nchi huru ya Kiafrika uliopatwa kutembelewa na shujaa wa Afrika, Nelson Mandela.
Na kuna Mtanzania anayeingia pia kwenye historia, ni Bw. John Mwakangale, huyu ni Mtanzania wa kwanza, akiwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya na kiongozi wa TANU , ambaye ndiye aliyempokea na kuongea rasmi na Nelson Mandela alipofika Mbeya.
Na pale hotelini Mbeya Mandela alishangazwa kuona kuwa hakukuwa na ubaguzi wa rangi kama ilivyo kwao Afrika Kusini. Mandela alibaini mara moja, kuwa amefika katika nchi inayotawaliwa na Waafrika weusi. Kwamba mzungu hakuwa mtu wa kuogopewa. Na hilo linathibitishwa pale bwana mmoja Mtanganyika mweusi, alipoona Mandela na mwenzake wanashangaa shangaa,  ndipo Mtanganyika yule alipokwenda sehemu ya mapokezi ya hoteli na kumwuliza mhusika, dada wa Kizungu;
“ Madam, did  Mr Mwakangale   inquire  after these two gentlemen” Aliuliza huku akiwaonyesha Mandela na Joe Matthews. Anasimulia Mandela.
Bwana yule Mtanganyika alimwuliza dada yule mhusika kwa vile alimwona  Mwakangale akifika hapo kuwaulizia wageni wake hao.
“ I am sorry, sir,’ – Samahani bwana, alisema dada yule na kisha akaendelea kusema;
“ He did, but I forgot to tell them”-  kwamba ni kweli Mwakangale amewaulizia, lakini nilisahau kuwaambia. Alisema dada yule mhudumu wa kizungu.
Bwana yule Mtanganyika akamalizia kwa kumwambia mhudumu;
“ Please, be careful, madam”-  Kwamba , tafadhali dada, uwe mwangalifu.
Ndipo hapo kwa maneno yake, Mandela anasimulia juu ya tukio hilo;
“  I then truly  realized that, I was in a country ruled by  Africans”- Kwamba ndipo kwa ukweli alipobaini, kuwa yuko kwenye nchi inayotawaliwa na Waafrika.

Na Mandela alijiona,  kwa mara ya kwanza maishani mwake,  kuwa yuko huru, mbali ya kwamba nyumbani kwao Afrika Kusini ni mtu anayesakwa kwa udi na uvumba na watawala.
 Hatimaye safari ya kutoka Mbeya kwenda Dar es Salaam ikawadia. Mandela akawasili Dar es Salaam siku ya pili yake.
Alipofika Dar es Salaam, Mandela akakutana na Julius Nyerere nyumbani kwake Msasani. Ndio,  ni Julius Nyerere, Rais kijana kwenye nchi ambayo ilikuwa na mwaka mmoja tu tangu ipate uhuru. Mandela alishangaa kuona Rais anakaa kwenye nyumba isiyo ya kifahari.   Alishangaa pia kumwona Rais anayeendesha mwenyewe gari yake. Mandela anasema;
“ I recall  that he drove  himself  in a simple  car,  a little  Austin”- Nakumbuka aliendesha mwenyewe gari ndogo ya kawaida aina ya Austin. ( Nelson Mandela, Long Walk To Freedom, pg. 345- 346)
Naam, ni yepi mengine yalimshangaza Mandela juu ya Nyerere alipokutana naye pale Msasani? Na je, waliongea nini?
Simulizi hii itaendelea…
0754 678 252
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top