Mjukuu wa mzee Mandela...Mandla Mandela alipokuwa akiongea na vyombo vya habari kijijini Mvezo jana.
*****
Chuki miongoni mwa familia ya Nelson
Mandela imeongezeka na kuchukua sura mpya jana pale mjukuu wa kiume na
mrithi Mandla kuwatuhumu ndugu zake kwa uzinzi na kuukamua umaarufu wa
kiongozi huyo anayeheshimika wa kupinga ubaguzi wa rangi.
Maoni yake hayo yamekuja wakati
mabaki ya miili ya watoto watatu wa kiongozi huyo mwenye miaka 94
ikizikwa upya kwenye eneo la makaburi ya awali kufuatia amri ya mahakama
kuirejesha baada ya Mandela kuwa amehamisha miili hiyo.
Katika mkutano na vyombo vya habari
uliorushwa moja kwa moja kwenye televisheni ambao umewafadhaisha
wananchi wa Afrika Kusini, Mandla alithibitisha tetesi kwamba mtoto wake
mdogo wa kiume, Zanethemba, alikuwa ni mtoto wa uhusiano haramu kati ya
kaka yake Mbuso na mke wa Mandla ambaye sasa wametengana, Anais
Grimaud.
Huku Mandela akiwa kwenye mashine ya
kupumulia hospitalini mjini Pretoria, chuki hiyo inayoongezeka
imeiduwaza na kuishitua Afrika Kusini kwa uwiano sawa.
"Mbuso alimpa ujauzito mke wangu,"
alisema Mandla huko Mvezo, kijiji kilichoko Eastern Cape kilomita 700
(maili 450) kusini mwa Johannesburg ambako Mandela alizaliwa na mahali
ambako Mandla anatumikia akiwa kama chifu rasmi wa ukoo huo.
Mandla, mwenye miaka 39, kwanza
aliibua maswali kuhusu ubaba wa mtoto wake mwaka jana wakati
alipotengana na Grimaud anayezungumza Kifaransa, ambaye tangu wakati huo
alirejea kwao katika kisiwa cha Reunion kilichoko kwenye Bahari ya
Hindi. Pia alibainisha wakati huo kwamba hakuwa na uwezo wa kupata
watoto.
Juhudi zake kuipata familia hiyo
kujibu maswali hayo ya ubaba wa Zanethemba yaligonga mwamba kwa lengo la
kuhifadhi mfanano wa umoja katika familia hiyo maarufu kabisa nchini
Afrika Kusini," alisema Mandla.
"Jambo hili halikuwahi kabisa
kujadiliwa na wanaoitwa ndugu wa familia hiyo ambao wanasema kwamba
wanataka kuhakikisha kwamba kuna utulivu katika familia hii," alisema,
akiwapa changamoto waandishi wa habari kufanya vipimo vya DNA
kuthibitisha madai yake hayo.
"Ukweli uko pale. Unaweza kwenda na
kubaini, fanya vipimo vya muhimu vinavyohitajika," alisema. Kaka yake
Mbuso amekana kuwa baba wa mtoto huyo.
Post a Comment