Mabingwa
wa soka wa Tanzania bara Dar es salaam Young African tayari
wamekwishaingia jijini Mwanza na leo wanataraji kushuka dimba la CCM
Kirumba kuvaana na KCC ya Uganda katika mechi ya kirafiki ya kimataifa.
Sambamba na Yanga timu ya KCC ambao ni mabingwa wa ligi ya nchini
Uganda nao tayari wamekwisha wasili salama mkoani hapa ambapo usiku wa
kuamkia leo waliandaliwa chakula cha pamoja na waandaaji wa mpambano huo
National Wide, iliyofanyika kwenye kiunga cha burudani Villa Park
Mwanza.
Sanjari na mchezo huo ambao unaonekana utakuwa na ushindani wa hali
ya juu kwa wenyeji Yanga kutaka kuwakosha mashabiki wao vilevile KCC
kutaka kudhihirisha kuwa wao ndiyo mabingwa wa Uganda taarifa toka
ungozi wa timu zote zinasema kuwa timu hizo zitatumia mchezo huo
kuonyesha zawadi na vikombe walivyotwaa kwenye ligi zao msimu
uliomalizika.
|
Wakipiga stori za hapa na pale Villa Park Mwanza. |
|
Benchi la Ufundi. |
|
Ni mazungumzo zaidi. |
|
Yanga. |
|
Baadhi ya wachezaji wa KCC. |
|
Eneo la tukio. |
|
Chating huku wakila muziki. |
|
Ufundi. |
Akizungumza na blogu hii Mwenyekiti wa Taasisi ya Michezo ya National
Wide Bw. John Kadutu, amesema kuwa mara baada ya mchezo wa leo dimba la
CCM Kirumba mabingwa hao watarudiana tena tarehe 7/07/2013 kutoa zawadi
ya sikukuu ya Sabasaba kwa wakazi wa Shinyanga.
Amevitaja viingilio katika michezo hiyo kuwa ni shilingi 3,000/= mzunguko na shilingi 10,000/= jukwaa kuu.
Ratiba zaidi inaonyesha kuwa ziara hiyo ya mabingwa itahitimishwa mkoani Tabora kwa Yanga Africans kumenyana na Mtibwa Sugar.
Yanga kwa mara ya mwisho walitimba mkoani Tabora enzi za wawakilishi
wa ligi kuu soka Tanzania bara, timu iliyoacha historia kwa kutandaza
soka safi Mirambo ya Tabora.
on Saturday, July 6, 2013
Post a Comment