Waziri wa
Kazi na Ajira, Gaudencia Kabaka akifungua Mkutano Mkuu wa tano wa wadau wa mfuko
huo ulifanyika jijini Arusha.
Mkurugenzi Mkuu wa PPF, Wiliam Erio akifuatilia mada
wakati wa mkutano huo.
Mkurugenzi
Mkuu wa GEPF, Daudi Msangi akifafanua jambo.
Mkurugenzi
Masoko na Uendeshaji wa GEPF, Ansilim Peter akitoa mada.
Meneja
Masoko na Utekelezaji, Aloyce Ntukamazina.
Wadau wa
mfuko wa GEPF.
Baadhi ya
wadau wakiwa katika mkutano huo.
Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Irene Isaka akizungumza
wakati wa Mkutano Mkuu wa tano wa Mwaka wa wadau wa Mfuko wa akiba ya
Wafanyakazi Serikalini (GEPF), jijini Arusha.
Mkuu wa ICT-SSRA, Dk. Carina Wangwe.
Mkuu wa ICT-SSRA, Dk. Carina Wangwe.
Mkurugenzi
Masoko na Uendeshaji wa GEPF, Ansilim Peter (kushoto) akibadilishana mawazo na
Meneja Masoko na Utekelezaji, Aloyce Ntukamazina.
Baadhi ya
wadau wakipata chai.
Wanamuziki
wa Marahaba Generation wakitumbuiza.
Waziri wa
Kazi na Ajira, Gaudencia Kabaka akifuatana na Mkurugenzi Mkuu wa GEPF, Daud
Msangi.
Wasanii wa
kikundi cha ngoma cha Watoto wa Simba cha jijini Arusha
kikitumbuiza.
Waziri wa
Kazi na Ajira, Gaudencia Kabaka akimsikili kwa makini Meneja Masoko na Utekeleza
wa Mfuko wa Akiba ya Wafanyakazi Serikalini (GEPF), Aloyce Ntukumazina mara
baada ya kufungua Mkutano Mkuu wa tano wa wadau wa mfuko huo ulifanyika jijini
Arusha.
Mbunge wa
Kigoma, Albert Obama akiwa na Mkurugenzi Mkuu wa GEPF, Daud Msangi katika
mkutano huo.
Wafanyakazi
wa Mfuko wa Akiba ya Wafanyakazi Serikalini (GEPF) wakiwa wamepozi kwa
picha.
Mkuu wa
Wilaya ya Arusha mjini, John Mongela akiagana na Meneja Masoko na Utekeleza wa
Mfuko wa Akiba ya wafanyakazi Serikalini (GEPF), Aloyce Ntukumazina mara baada
ya kufungua Mkutano Mkuu wa tano wa wadau wa mfuko huo ulifanyika jijini Arusha.
Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa GEPF, Daud Msangi, Mbunge wa Kigoma, Albert Obama
na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Joyce Shaidi.
Picha ya
pamoja.
Na
Mwandishi Wetu
Mifuko ya
Hifadhi za Jamii imeaswa kuwekeza katika vitega uchumi vyenye tija ili mifuko
hiyo iweze kuwa endelevu na kutoa huduma bora kwa
watanzania.
Hayo
yameelezwa na Waziri wa Kazi na Ajira Gaudencia Kabaka alipokuwa akizungumza
katika mkutano wa 10 wa Mfuko wa Akiba ya Wafanyakazi wa serikalini (GEPF)
uliofanyika jijini hapa.
Gaudencia
Kabaka alisema kuwa mifuko hiyo iwekeze zaidi katika vitega uchumi ili kuepuka
kufilisika na kuweza kujiendesha yenyewe kwa faida na kuwanufaisha wanachama
wao.
Pia
amewataka wananchi kujiwekea akiba itakayowasaidia kukabiliana na majanga ya
kiuchumi na kijamii yanayotokea katika maisha.
“Ni vizuri
wananchi wakahamasishwa kujiwekea akiba itakayowasaidia kipindi cha
uzeeni,wanapokubwa na maradhi ama ulemavu kwasababu hatujui leo unaweza kuwa
mzima una nguvu na kesho hauna nguvu ndio maana tunasema hatujui ya kesho
unaweza kuwa mlemavu mtarajiwa ama marehemu mtarajiwa” alisema Waziri
Kabaka.
Waziri
kabaka ameitaka mifuko hiyo kuacha kugombania wanachama walioajiriwa tu badala
yake wapanue wigo na kuwaendea watu walioko katika sekta zisizo
rasmi.
Naye
mkurugenzi wa mfuko huo wa [GEPF) Daudi Msangi alisema kuwa mfuko huo una lengo
la kuhakikisha kuwa watu waliojiajiri wanaingia kwa wingi katika mfuko huo
.
“Changamoto
kubwa tuliyonayo ni wananchi kutokuwa na uelewa wa kutosha juu ya kuhusiana na
mifuko ya jamii wengi wanadhani wanapoteza fedha jambo ambalo halina ukweli
bali mifuko hiyo inawasaidia kujiwekea akiba kwa ajili ya sasa na ya maisha ya
badae” Alisema Mkurugenzi huyo.
Post a Comment