Picha ya pamoja na viongozi wa Halmashauri ya jiji la
Mwanza.
Sehemu ya vyandarua vilivyotolewa msaada vikiwa tayari
vimefungwa na wasanii wa filamu hapa nchini,mara baada ya kutoa msaada wa
vyandarua hivyo ndani ya wodi ya wazazi kwenye hospitali ya Mkoa wa jiji la
Mwanza-Sekou-toure mapema leo asubuhi kwa
udhamini mkubwa wa kinywaji kisicho na kilevi cha
Grandmalt..
Msanii wa Bongo Movie,Jacline
Wolper akiwa katika wodi ya wazazi ,Hospital ya Mkoa wa Mwanza Sekou-toure
akifunga chandarua kwenye moja ya vitanda hospitalini hapo,ikiwa ni sehemu ya
vyandarua vilivyotolewa na wasanii hao kupitia kinywaji cha
Grandmalt
Wasanii Irine Uwoya na Shamsa
Ford wakiwa na mmoja wazazi akiwa amembeba mtoto aliezaliwa kwenye hospitali
hiyo ya Mkoa wa Mwanza, Sekou-toure mara baada ya wasanii hao
kutembelea Hospitali hiyo na kutoa vyandarua kwenye wodi
Wazazi.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya jiji la Mwanza,Halifa
Hassan Hida akizungumza machache (mbele ya wasanii wa Bongo Movie (hawapo
pichani) ikiwemo na kuwashukuru wasanii hao wa filamu kwa kitendo cha kiungwana
kabisa katika suala zima la kuisaidia jamii yao inayowazunguka kwa njia moja ama
nyingine na pia amewataka kuwasaidia wasanii wachanga wa jiji la Mwanza na
kuwaelekeza njia sahihi za mafanikio katika tasnia hiyo ambayo kwa sasa imezidi
kushika kasi siku siku.
Meneja wa kinywaji cha Grandmalt
Consolata Adam akipokea mkono wa shukurani kutoka kwa katibu wa Afya hospitali
ya Sekou-toure
Bwa.Daniel Temba,mara baada ya kabidhi msaada wa vyandarua
sanjari na wasanii mbalimbali wa filamu,makabidhiano hayo yamefanyika mapema leo
kwenye hospitali ya mkoa wa Mwanza Sekou-toure,ikiwa ni sehemu ya wasanii hao
kuwa karibu na wananchi, kisha baadae kuonyesha kazi zao mbalimbali kwenye
uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza.
Wasanii mbalimbali wakiongozwa na
Raymond Kigosi wakikabidhi msaada wa vyandarua
kwenye hospitali ya mkoa wa Mwanza Sekou-toure, kwa katibu wa afya wa Hospitali
hiyo Bwa.Daniel Temba ikiwa ni sehemu ya wasanii hao
kuwa karibu na wananchi, kisha baadae kuonyesha kazi zao mbalimbali kwenye
uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza.
wasanii wakiendelea na zoezi
la wakikabidhi msaada wa vyandarua
kwenye hospitali ya mkoa wa Mwanza Sekou-toure kwa katibu wa afya wa
Hospitali hiyo ikiwa ni sehemu ya wasanii
hao kuwa karibu na wananchi, kisha baadae kuonyesha kazi zao mbalimbali kwenye
uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza.
Baadhi ya wasanii wa Filamu hapa nchini a.k.a Bongo
Movie Unity wakiwasili kwenye hospitali ya Sekou-toure tayari kwa kushiriki
zoezi la kugawa vyandarua kwenye wodi ya wazazi kwa udhamini mkubwa wa kinywaji
kisicho na kilevi cha GrandMalt mapema leo
asubuhi.
Mlezi wa Bongo Movie Unity,Jacob Steven a.k.a JB a.k.a
Bonge la Bwana wakisalimiana na Afisa mhausiano wa Halmashauri ya jiji la
Mwanza,Bwa.Joseph Mlinzi,pichani kati ni msanii wa filamu Singo
Mtambalike.
Baadhi ya Wasanii hao wa Bongo Movie Unit wakitoka
kwenye wodi ya Wazazi mara baada ya kukabidhi msaada wa vyandarua vilivyotolewa
kwa hisani kubwa ya kinywaji kisicho na kilevi cha
Grandmalt.
====== ======= =========
Wasanii Tamasha la Filamu Grand Malt watoa
msaada
Na Mwandishi Wetu, Mwanza
WASANII maarufu wa Bongo Movie hapa nchini, ambao wapo
hapa kwa ajili ya Tamasha la Wazi la Filamu Tanzania, maarufu kama ‘Grand Malt
Tanzania Open Film Festival’ jana walikabidhi vyandarua kwa Halmashauri ya Jiji
la Mwanza pamoja na Hospitali ya Rufaa ya Sekou Toure.
Akizungumza na wasanii hao, Mkurugenzi wa Jiji la
Mwanza, Halifa Hassan Hida, aliwashukuru wasanii hao kwa msaada huo na kuwataka
wawasaidie pia wasanii wachanga wa jijini hapa ili nao waweze
kutoka.
“Nimefarijika na msaada huu pamoja na ujio wenu, ila
kimoja ninachokiomba kutoka kwenu ni kuwasaidia wasanii wa Mwanza ili nao waweze
kutoka, naamini ujio wenu ni changamoto kubwa kwao,” alisema
Hida.
Kaimu Meya wa Jiji la Mwanza, Dismas Masuni naye alitoa
shukrani kwa msaada huo na kusema wapo ni vema zaidi kwa wasanii hao pia
kufikiria kuwekeza jijini hapa kwa ajili ya maendeleo
yao.
Meneja wa kinyawaji cha Grand Malt, Consolata Adam,
alisema nia kubwa ya kuamua kudhamini tamasha hilo ni kuwaendeleza zaidi vijana
kwani wengi wako katika ajira hiyo na kutaka wakazi wa Mwanza kufika kwa wingi
wakati wote wa tamasha hilo.
Wakati walipokabidhi msaada wa vyandarua katika
hospitali ya rufaa ya Sekou Toure na kuvifunga katika wadi ya wazazi, wasanii
hao walionekana kuguswa zaidi na hali ilivyo na kusema wana jukumu kubwa la
kuisaidia jamii. Katibu wa Afya wa hospitali hiyo, aliye pia kaimu Katibu wa
Afya wa Mkoa, Danny Temba alishukuru kwa msaada huo na kusema umekuja wakati
muafaka kutokana na mahitaji yaliyopo.
“Tunashukuru mno kwa msaada wenu na kwa kutaka
kuwadhihirishia tuna mahitaji makubwa na vyandarua hasa katika kupambana na
malaria, naomba mkavifunge wenyewe,” alisema Temba, ombi lililoridhiwa na
wasanii hao na kuomba wavifunge katika wadi ya mzazi na
mtoto.
Wasanii walionekana kuguswa zaidi walipoingia katika
wadi hiyo, huku Jacqueline Wolper, Shamsa Ford, Chuchu Hans, Aunty Ezekiel,
Vicent Kigosi ‘Ray’, Hashim Kambi na wengineo wakionekana kuguswa zaidi na
mahitaji ya wadi hiyo.
“Kuna mahitaji makubwa katika hospitali hii, kuna kitu
kimenigusa mno kwa kuja hapa,” alisema Jacob Steven ‘JB’, huku akiungwa mkono na
Single Mtambalike ‘Ritchie Ritchie’ na Steve Nyerere.
Mratibu wa Tamasha hilo, Musa Kissoky, ambalo
lilizinduliwa rasmi jana katika Uwanja wa Nyamagana alisema, kutakuwa na filamu
za aina mbalimbali zitakazoonyeshwa wakati wote wa tamasha
hilo.
Kissoky alisema, tamasha
hilo ambalo litakuwa la bure kwa watu wote na kushirikisha mastaa wa filamu hapa
nchini, litakuwa la aina yake na kuwataka wakazi wa Mwanza wajitokeze kwa wingi
kushuhudia mambo yanayoendelea.
Meneja wa kinywaji cha
Grand Malt walio wadhamini wakuu wa tamasha hilo, Consolata Adam, alisema
wameamua kufanya kweli zaidi kwani wanataka kuona Watanzania wanapata kitu
chenye uhakika. “Tumejipanga katika hili na
wala hatutanii. Tunawakaribisha watu wote wenye mapenzi na filamu zetu za
Tanzania kufika na kushuhudia tamasha hili ambalo mwaka huu limeboreshwa zaidi,”
alisema Consolata.
Tamasha hilo la filamu
limedhaminiwa na kinywaji cha Grand Malt kisicho na kilevi ambacho kinazalishwa
na kusambazwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL).
Post a Comment