Mstahiki
Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa akiwasili katika viwanja vya
maonyesho ya 37 ya Kimataifa ya Biashara Sabasaba yanayoendelea jijini
Dar ambapo alitembelea mabanda mbalimbali.(Picha na Zainul Mzige).
Mkurugenzi
Mtendaji wa Home Shopping Centre (HSC) Fahad Said Mohamed (kushoto)
akimkaribisha Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa kwenye
Banda la HSC kwenye maonyesho ya 37 kimataifa ya Biashara yanayoendelea
katika uwanja wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam.
Mstahiki
Meya Jerry Silaa akiangalia baadhi ya bidhaa zenye ubora zinazouzwa na
Kampuni ya HSC katika maonyesho ya 37 ya Kimataifa ya Biashara katika
viwanja vya Sabasaba jijini Dar. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Home
Shopping Centre (HSC) Fahad Said Mohamed.
Mstahiki
Meya Jerry Silaa akingalia kifaa cha kusafishia mazulia jinsi
kinavyofanya kazi. Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Home Shopping
Centre (HSC) Fahad Said Mohamed.
Mstahiki
Meya Jerry Silaa akiwa kwenye picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa
Home Shopping Centre (HSC) Fahad Said Mohamed na baadhi ya wafanyakazi
wa HSC katika Banda lao lililopo kwenye viwanja vya Sabasaba.
Umati
wa wakazi wa jijini Dar es Salaam ukiwa umefurika kwenye Banda la Home
Shopping Centre kujipatia mahitaji mbalimbali ya nyumbani.
Mtsahiki
Meya Jerry Silaa akipewa maelezo ya jinsi Mfuko wa Fursa sawa kwa wote
unavyopambana na kutokomeza Ugonjwa wa Saratani ya Matiti kwa wakina
mama nchini. Kushoto ni Mwenyekiti wa Mfuko wa Fursa Sawa kwa
Wote (EOTF) Mama Anna Mkapa.
Mstahiki
Meya Jerry Silaa akisalimiana Mke wa Makamu wa Rais Mama Asha Bilal
walipokutana kwenye Banda la Mfuko wa Fursa sawa kwa wote (EOTF) kwenye
viwanja vya maonyesho ya Kimataifa ya Biashara jijini Dar.
Mwenyekiti
wa Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote (EOTF) Mama Anna Mkapa akiagana na
Mstahiki Meya Jerry Silaa mara baada ya kutembelea Banda la (EOTF)
linalotoa fursa kwa wajasiriamali nchini Tanzania kuonyesha bidhaa zao
katika maonyesho hayo kila mwaka.
Mstahiki
Meya Jerry Silaa akipata maelezo jinsi ya kutumia Kizimamoto Fanisi cha
kurusha (Fire Extinguisher) ambacho ni rahisi kutumia na hakihitaji
matengenezo na hudumu kwa miaka mitano pia Kifaa hicho ni rafiki wa
mazingira na mvumbuzi bora kwa uokoaji wa dharura wakati alipotembelea
Banda la GreenBat Fire Solutions katika maonyesho ya Sabasaba
yanayoendelea.
Mstahiki Meya Jerry Silaa katika picha ya pamoja na Wakurugenzi wa GreenBat Fire Solutions.
Mstahiki
Meya Jerry Silaa akisaini kitabu cha wageni katika banda la Arusha
International Conference Centre (AICC) wanaoshughulika kutoa huduma za
kumbi za Kimataifa za mikutano na Utalii jijini Arusha.
Mstahiki
Meya Jerry Silaa akingalia jinsi mtoto Range Jackson ( wa pili kushoto)
mwenye ulemavu wa Ubongo akionyesha ramani ya Tanzania na Sehemu ya
mipaka yake iliyotumika kumfundishia kujua kusoma na kuandika na ufundi
stadi kupitia kituo cha VETA. Kulia ni Mkufunzi wa kuchomea (Welding
Instructor) na Mwalimu wa watu wenye mahitaji maalum Bw. Kintu Kilanga
na Wa tatu kulia ni Baba mzazi wa kijana huyo Bw.Jackson Range.
Post a Comment