Mratibu wa shindano la Redd’s Miss Temeke Benny Kisaka
akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusu shindano la
Redd’s Kanda ya Temeke linalotarajiwa kufanyika katika ukumbi wa TCC Club
Chang'ombe Julai 5. Kulia ni Mkuu wa Itifaki wa Kamati ya Miss Tz, Albert
Makoye.
Mkuu
wa Itifaki wa Kamati ya Miss Tanzania, Albert Makoye akizungumza kuhusu fainali
ya Redd's Miss Temeke.
Na
Mwandishi Wetu
MREMBO
atakayetwaa taji la Redds Miss Temeke 2013, linalofanyika Ijumaa Julai 5, mwaka
huu ataondoka na zawadi za jumla ya Sh. Milioni 3,250,000 ikiwa ni zawadi kubwa
zaidi kutolewa katika mashindano yote ya urembo, yaliyofanyika mwaka
huu.
Mshindi
huyo, atapata ofa ya mwaka mzima kutoka RIO gym & Spa, iliyopo Quality
Center, kutumia vifaa vyote ndani ya gym hiyo ambayo gharama yake ni Milioni
1,400,000, pia atajinyakulia simu ya kiganjani yenye thamani ya Sh 700,000 ,
dinner set kutoka AKO Catering yenye thamani ya Sh,150,000 sanjari na pesa
taslim Sh. Milioni 1, hiyo jumla yake ni Milioni
3,250,000.
Mshindi wa
pili katika mashindano hayo ambayo mgeni rasmi atakuwa Mbunge wa Jimbo la
Temeke, Abas Mtemvu atajinyakulia kitita cha Sh.800,000 pesa taslim na dinner
set ambayo thamani yake ilikuwa bado haijathibitishwa na mdhamni wa zawadi hiyo
wakati mshindi wa tatu ambao wote kwa pamoja ni wawakilishi wa Miss Temeke, yeye
atajipatia fedha taslimu Sh 700,000.
Sh ,
400,000 zitakwenda kwa mshindi wa nne na atakayeshika nafasi ya tano yeye
ataibuka na Sh 300,000. Washiriki wengine ambao hawatabahatika kuingia katika
nafasi ya tano bora, wote watapewa Sh,200,000 kwa maana ya kifuta
jasho.
Tumelenga
zawadi za fedha zaidi, hii ni kutokana na ugumu wa maandalizi kwa warembo ambao
hugharamika zaidi, kiasi nasi kuona kuna kila namna ya kuwapunguzia maamivu
hayo.
Shindano
hilo, linatarajiwa kuwa na burudani ya kipekee kutoka kwa mshindi wa tungo bora
ya Bongo Fleva ya Kili Music mwaka huu, Ben Paul sanjari na Twanga Pepeta ambayo
mwishoni mwa wiki, ilizindua albamu yake ya 13 kwa mafanikio
makubwa.
Warembo
watakaopanda jukwaani Julai 5 ni kutoka Kigamboni, Kurasini na Chang'ombe ambao
wanawania taji linaloshikiliwa na Miss Tanzania namba tatu, Edda Sylvester
walikuwa chini ya wakufunzi Suzy Mwenda na Shadya Mohamed wakati kwenye kucheza
nako walikuwa na walimu wawili Super Bokilo na
Charles.
Warembo hao
ni pamoja na Axsaritha Vedastus, Darling Mmary, Esther Muswa, Hyness Oscar,
Irene Rajab, Jamila Thomas, Latifa Mohamed, Margreth Gerald, Margreth Olotu, Mey
Karume, Mutesi George, Naima Ramadhan, Narietha Boniface , Stella Mngazija na
Svtlona Nyameyo
.
Shindano
hilo limedhaminiwa na kinywaji cha Redd's, Dodoma Wine, Gazeti la Jambo Leo,
Cloud’s Media, Blogu ya Wananchi (Le Mutuz), Fredito Entertainment, CXC Africa
tours & Safaris, RIO Gym & Spa, 100.5 Times FM na Kitwe General
Traders.
Mbali ya
wadhamini hao pia Redds Miss Temeke imechangiwa katika ufanikishaji na Mbunge wa
Jimbo hilo, Abbas Mtemvu na mwanamichezo maarufu nchini Geofrey Nyange Kaburu
hasa kwa upande wa zawadi.
Temeke,
imewahi kutoa warembo kadhaa miaka ya nyuma waliopata mafanikio katika
mashindano hayo, mitindo na kazi nyingine hasa kupata uzoefu wa kujiamini katika
njanja mbalimbali. Miongoni mwao ni Miriam Odemba(1997) aliyepata kuiwakilisha
Tanzani katika fainali za mitindo zilizofanyika Nice Ufaransa na kupata mkataba
wa Elite Model Look, baadaye kufakinikiwa kutwaa nafasi ya pili ya Miss Earth
World, zilizofanyika China.
Pia, Temeke
ilimtoa Happines Millen Magesse(2001), na kutwaa taji la Miss Tanzania na kwa
sasa anang'ara sana katika tasnia ya mitindo katika nchi za Marekani, Afrika
Kusini na barani Afrika kwa ujumla. 2003 Temeke ilimtoa Miss Tanzania, Sylvia
Bahame na 2006 kuwatoa Jokate Mwegelo na Irene
Uwoya.
Jokate
alitwaa taji la Miss Temeke mwaka huu na pia kushika nafasi ya pili Miss
Tanzania na pia kushinda taji la ubalozi wa Redd's na gazeti la Citizen. Uwoya
ambaye alikuwa mshindi wa pili Temeke alishika nafasi ya nne kwenye Miss
Tanzania mwaka huo. Genevieve Mpangala mwaka 2010 alitwaa taji la Miss Temeke
baadaye kushinda taji la Miss Tanzania.
Nafasi
nyingine za juu zilizowahi kutwaliwa na warembo kutoka Temeke ni pamoja na Irene
Kiwia, mshindi wa nne Miss Tanzania mwaka 2000, Regina Mosha mshindi wa nne Miss
Tanzania mwaka 2002, Cecylia Assey mshindi wa pili Miss Tanzania 2004, Queen
David mshindi wa tatu mwaka 2007 na Edda Sylvester mshindi wa tatu Miss Tanzania
akiwa anashikilia taji la Redds Miss Temeke.
BMP
Promotions inayoandaa mashindano haya kwa mwaka wa 18 sasa, inatanguliza
shukrani zake wadhamini wetu kwa miaka hiyo, sanjari na vyombo vyote vya habari
kwa ujumla wake, kwani ndio waliofanikisha kuandaa Miss Temeke kwa ufanisi
katika muda wote huo, shukrani sana.
Post a Comment