IGP Mwema


...................................................................................

Na Esther Macha,Makete

JESHI la polisi wilayani Makete mkoani Njombe limewataka wamiliki wa nyumba za kulala wageni wilayani hapa kuhakikisha wanaandikisha na kutunza taarifa za wageni wanaofika kulala kwenye nyumba hizo, ili ziweze kusadia pindi kunapotokea tatizo
Wito huo ulitolewa na Mkuu wa polisi wilaya ya Makete SP Peter Kaiza wakati akizungumza na wamiliki na wahudumu wa nyumba hizo katika kikao kilichofanyika kwenye ukumbi wa halmashauri ya wilaya hiyo kuhusiana na tabia ya baadhi ya wahudumu wa nyumba za kulala wageni .


“Ikitokea mgeni amekuja kulala kwenye nyumba unayofanyia kazi, wewe hujampa daftari akandika jina na taarifa zingine, usiku linatokea la kutokea mtu ananyooka(anakufa) sasa utajibu nini kwa bosi wakao na kuja kutoa taarifa polisi utaanza anza je;?Kaiza aliwahoji wa hudumu hao.
Katika hatua nyingine Kaiza alisema kuwa kutokana na dhana iliyojengeka miongoni mwa wahudumu hao kuwa wateja wengi huandika taarifa za uongo hivyo kuona hakuna haja ya kuandika taarifa zao akisema si kweli kuwa kila taarifa itakuwa ya uongo na kusisitiza kuwa wawaandikishe kwa kuwa zitasaidia pindi likitokea tatizo
Aidha kwa upande wake Ofisa biashara wilaya ya Makete Adonia Mahenge aliwa taka washudumu wahudumu wa afya wakatambua umuhimu wa kutunza taarifa hizo kwani ni suala la kisheria ambalo linatakiwa kufuatwa na kila mhudumu wa nyumba ya kulala wageni
Alisema kutokana na hali hiyo watakuwa wanafanya ukaguzi muda mara kwa mara ili kuona kama hatua hizo zinafuatwa na kwamba ambaye atakuwa amekiuka utaratibu atachukuliwa hatua kali za kisheria, ni vema wahudumu hao na wamiliki waweke mabango yanayoonesha utaratibu na kanuni na masharti ya kulala kwenye nyumba za wageni.

Alisema kuwa maazimio hayo yanatakiwa kufuatwa na wahudumu pamoja na wa,iliki ndani ya wilaya nzima ya Makete ikiwemo Makete mjini, Ikonda, Bulongwa, Matamba na maeneo mengine ambayo nyumba hizo zipo

 Imechotwa: Matukio Daima Blog