Mtaalamu wa mazingira wa
ofisi ya bonde la maji la Pangani ,Mhandisi Arafa Maggidi akiwa na mtaalamu wa
vipimo kutoka kituo cha utafiti wa kuondoa Frolide cha Ngurdoto Godfrey Mkongo
wakiangalia maji yanayodaiwa kuwa na kemikali yakiingia mto Karanga
.
Mtaalamu wa mazingira wa
ofisi ya bonde la maji la Pangani ,Mhandisi Arafa Maggidi akiwa na mtaalamu wa
vipimo kutoka kituo cha utafiti wa kuondoa Frolide cha Ngurdoto Godfrey Mkongo
wakichukua sampuli ya maji ya Mto Karanga kwa ajili ya
vipimo.
Mwananfunzi wa chuo cha
maabara ya sayansi,ufundi na teknolojia Arusha Stephew Msalale akichukua maji ya
mto Karanga kama sampuli kwa ajili ya vipimo.
Mtaalamu wa mazingira wa
ofisi ya bonde la maji la Pangani ,Mhandisi Arafa Maggidi akiwa na mtaalamu wa
vipimo kutoka kituo cha utafiti wa kuondoa Frolide cha Ngurdoto Godfrey Mkongo
wakichukua sampuli ya maji ya Mto Karanga kwa ajili ya
vipimo.
Na Dixon Busagaga waglobu
ya jamii Moshi
KUFUATIA kutolewa kwa
taarifa za kutiririshwa kwa maji yanayodaiwa kuchanganyika na kemikali kutoka
kwa baadhi ya viwanda vilivyoko kando ya mto Karanga ofisi ya Bonde la
Pangani(PBWO) imelazimika kuchukua sampuli ya maji hayo kwa ajili ya kuyafanyia
vipimo.
Hatua hiyo imekuja siku
chache baada ya taarifa za kichunguzi zilizofanywa na Globu ya jamii baada ya
kuwezeshwa na na mfuko wa waandishi wa habari(TMF) na kuripoti jinsi wakazi wa
vijiji vya Chekeereni,Weruweru,Mijongweni na Kiyungi walivyo athirika na maji
hayo.
Wataalamu wa vipimo vya
maji Godfrey Mkongo na Steven Msalale mwanafunzi wa mwaka wa pili wa chuo cha
ufundi,maabara ya sayansi na teknolojia wakiwa wameambatana na mtaalamu wa
mazingira kutoka Bonde la maji la Pangani walifika katika mto huo kuchukua
vipimo.
Jumla ya sampuli saba
zilichukuliwa kutoka katika maeneo matatu tofauti ambayo yanadaiwa maji yake
kuwa na madhara yanayo sababisha magonjwa mbalimbali kwa wakazi wa vijiji hivyo
vilivyoko wilaya ya Moshi vijijini.
Maeneo ambayo maji yake
yalichukuliwa sampuli ni pamoja na kabla na baada ya daraja la Bonite ambako
kunafanyika shughuli za uoshaji wa Karoti kutoka katika mashamba yaliyoko
Weruweru kabla ya kusafirishwa kupelekwa kwenye masoko ya ndani na nje ya mkoa
wa Kilimanjaro.
Kwingine kulikochukuliwa
sampuli ya maji ni eneo la daraja la gari Moshi ambako kuna maingilio makubwa ya
maji ambayo yanatiririka kutoka katika viwanda vya Kibo paper na China paper
yanayodaiwa kuwa na kemikali .
Sampuli ya maji
iliyochukuliwa katika eneo hilo ni ile ya maji yatokayo katika maingilio ya
kwainda cha Kibo Paper peke yake ,kasha ikachuliwa pia sampuli ya maji yatokayo
katika maingilio ya kiwanda cha China paper.
Maeneo mengine ambayo maji
yake yalichukuliwa sampuli ni pamoja na mbele ya daraja la gari Moshi eneo
ambalo wananchi wengi wamekuwa wakifanya shughuli za kuoga kuosha vyombo pamoja
na kufua nguo.
Eneo la mwisho ambako maji
yake yalichukuliwa sampuli ni eneo kilipo kiwanda cha viberiti cha Kibo(Kibo
match) ambacho pia yapo madai kuwa kiwanda hicho licha ya kuwa na eneo maalumu
la kuhifadhia maji yake huenda yakawa yanapita chini ya
ardhi.
Sampuli hizo zote
zilipelekwa kituo cha utafiti wa viuatilifu nchini (TPRI) kilichopo jijini
Arusha ambako mbali na vipimo vya kemikali zilizoko ndani ya sampuli hizo pia
kulifanyika vipimo vya kujua endapo maji hayo yana bacteria wanao sababisha
magonjwa mbalimbali kwa binadamu.
Akizungumzia zoezi hilo
mtaalamu wa mazingira ofisi ya Bonde la maji la Pangani Arafa Maggidi alisema
vipimo vingine vilipelekwa kituo cha utafiti wa kuondoa Frolide iliyopo Ngurdoto
na vingine maabara kuu ya maji iliyopo Dar es salaam.
Alisema hadi sasa majibu ya
vipimo hivyo kutoka katika maabara zote tatu hayajarejeshwa hali inayochangia
hadi sasa ofisi hiyo kuendelea kuchukua hatua zaidi katika mto huo ili kuokoa
wakazi wa maeneo ya vijiji vya Chekereni,Weruweru,Mijongweni na Kiyungi
wanaoendelea kuyatumia maji hayo hadi sasa.
Post a Comment