Rais
wa Marekani, Barack Obama na mkewe Michelle, wakipanda ndege yao aina
ya Air Force One, tayari kuondoka nchini kurejea nchini kwao baada ya
kumaliza rasmi ziara yao katika Bara la Afrika, ambapo amemalizia ziara
hiyo kwa kufanya ziara ya siku mbili nchini Tanzania. Obama na msafala
wake ameondoka leo mchana.
Rais
Obama na mkewe, wakipunga mikono kuwaaga wenyeji wao Rais Jakaya
Kikwete na mkewe, Viongozi wa Kiserikali na wananchi waliofika uwanjani
hapo kuwaaga leo, mchana wakati wakiondoka nchini.
Rais
Jakaya Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete, wakipunga mikono kuwaga
wageni wao Rais Obama na mkewe wakati wakiondoka nchini leo mcahana
baada ya kumaliza ziara yao.
Rais Jakaya Kikwete, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Sadick na Balozi wa Marekani nchini, Alfonso (kulia) wakiipungia ndege iliyokuwa inapaa.
Rais
Barack Obama akiagana na Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es salaam huku
Mstahiki Meya wa Ilala pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe.
Liberata Mulamula wakisubiri zamu zao.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete na Rais Barack Obama wakipokea saluti wakati
nyimbo za Taifa zikipigwa wakati wa kuondoka kwa Rais huyo wa Marekani
leo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere. Nyuma yao ni
Mama Salma Kikwete na Mama Michelle Obama pamoja na Mkuu wa majeshi
Jenerali Davis Mwamunyange pamoja na IGP Saidi Mwema . Kushoto ni Mkuu
wa Itifaki Balozi Mohamed Maharage na Mkuu wa Itifaki wa Ikulu ya
Marekani (White House) Balozi Capricia Marshall. Ziara ya Rais Obama
nchini imetajwa kuwa moja ya ziara za viongozi wa nje zilizofanikiwa
sana, ambapo maelfu ya Watanzania walijitokeza kumlaki na kumuaga.
CREDIT: SUFIANI MAFOTO BLOG
Post a Comment