MCHUNGAJI wa Kanisa la
Evangelical Assemblies of God of Tanzania(EAGT) la Iwambi Jijini Mbeya Daniel
Mwasumbi akiwa mahakamani kungojea kesi
yake.
Wananchi Mbalimbali wakisubiri Kusikiliza Kesi ya
MCHUNGAJI wa Kanisa la Evangelical Assemblies of
God of Tanzania(EAGT) la Iwambi Jijini Mbeya Daniel
Mwasumbi
MCHUNGAJI wa Kanisa
la Evangelical Assemblies of God of Tanzania(EAGT) la Iwambi Jijini Mbeya Daniel
Mwasumbi aliye vaa koti Jeupe akiwa anatolewa mahakamani Baada ya kusomewa
kifungo cha Miaka 30 Jela
Watoto wa MCHUNGAJI
wa Kanisa la Evangelical Assemblies of God of Tanzania(EAGT) la Iwambi Jijini
Mbeya Daniel Mwasumbi wakiwa wanatoka Mahakamani Baada ya Baba yao kusomewa
kifungo
Mtoto wa MCHUNGAJI wa
Kanisa la Evangelical Assemblies of God of Tanzania(EAGT) la Iwambi Jijini Mbeya
Daniel Mwasumbi akiwa anaongeaa na waandishi wa Habari baada ya kesi
kumalizika
Waumini Mbalimbali wakiwa nje Baada ya kesi kumalizika
Watoto wa MCHUNGAJI wa Kanisa la Evangelical Assemblies of God of Tanzania(EAGT) la Iwambi Jijini Mbeya Daniel Mwasumbi wakiwa nje hawaamini baada ya kusikia Baba yao anafungwa Miaka 30 |
Binti anaye daiwa kufanyiwa kitendo hicho akilia kwa
Uchungu baada ya kesi kwisha
***********
MCHUNGAJI wa Kanisa
la Evangelical Assemblies of God of Tanzania(EAGT) la Iwambi Jijini Mbeya Daniel
Mwasumbi amehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela na viboko 12 baada ya kukutwa na
makosa mawili ya Kubaka na kumpa mimba Mwanafunzi wa miaka
19.
Akisoma hukumu hiyo
Hakimu wa mahakama ya Wilaya ya Mbeya Ndugu Gilbert Ndeuruo amesema Mahakama
imemta hatiani kutokana na ushahidi uliotolewa na Shahidi namba moja katika kesi
hiyo ambaye ni mhanga wa tukio hilo Neema
Beni(19).
Amesema Mtuhumiwa
huyo ilidaiwa kutenda makosa hayo kati ya Mwezi Januari 2008 hadi Mwaka 2011
katika eneo la Iwambi kinyume na Sheria kifungu cha 130(2)e na 131 (1) sura ya
16 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2002 kwa kosa la
ubakaji.
Kutokana na ushahidi
huo Hakimu Ndeuruo alidai kuwa Mahakama yake imemkuta Mtuhumiwa na makosa mawili
ya Ubakaji na kumpa ujauzito kwa ushahidi uliotolewa na Mhanga mwenyewe pamoja
na Mwalimu wa Shule aliyokuwa akisoma ambapo alidai kuwa Shtaka limedhihirishwa
pasipo shaka chini ya kifungu cha 235/1985.
Kwa upande wake
Mwendesha mashtaka wa Serikali Archiles Mulisa aliiomba Mahakama hiyo kutoa
adhabu kali kutokana nan mtuhumiwa kutenda kosa la kinyama tofauti na umri wake
na wa binti ambapo Binti anaumri wa Miaka 19 ili hali Mtuihumiwa akiwa na Miaka
57.
Pia alidai kuwa
Mtuhumiwa huyo alimwalibia masomo na maisha yake binti huyo na vitendo hivyo
alikuwa akivifanyia sehemu mbali mbali ikiwemo kanisani hivyo aliiomba mahakama
hiyo kuvitaifisha na kutoa amri ya Matunzo ya Watoto kwa kutumia amri ya
kutaifisha malishtakiwa.
Hata hivyo Hakimu
alimuuliza Mtuhumiwa kupunguziwa adhabu ambapo Mshtakiwa huyo aliomba
kupunguziwa adhabu kwa madi kuwa ameachiwa watoto na ndugu zake aliozaliwa nao
wakiwemo wazazi wake hivyo akifungwa hawatakuwa na
msaada.
Aidha kutokana na
utetezi huo Hakimu Ndeuruo alimhukumu kifungo c ha Miaka 30 na viboko 12
kutokana na kosa la kwanza ili hali katika kosa la pili amehukumiwa kifungo cha
Miaka 5 na kuongeza kuwa adhabu hizo zitaenda kwa pamoja na kulipa fidia ya
Shilingi Milion 20 kwa fedha za Tanzania kwa familia ya
Mhanga.
Ameongeza kuwa
Mtuhumiwa anahaki ya kukata rufaa katika Mahakama kuu ya Mbeya kama hatakuwa
ameridhika na adhabu aliyopewa na mahakama yake.
Habari ,Picha na
Mbeya yetu Blog
Post a Comment