Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

RC DODOMA APEWA MIZINGA 85 YA KUFUGIA NYUKI NA KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA

 


PIX 1

Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini, Kamishna Jenerali John Minja akimkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk Rehema Nchimbi (kushoto) katika hafla maalumu ya makabidhiano ya mizinga ya nyuki 85 iliyotengenezwa na jeshi hilo ambayo itatumika kufugia nyuki katika Mkoa wa Dodoma. Hafla hiyo imefanyika katika Viwanja vya Gereza Kuu Isanga, mjini Dodoma. PIX 2
Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini, Kamishna Jenerali John Minja akitoa hotuba fupi ya kumkaribisha mgeni rasmi, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk Rehema Nchimbi kabla ya makabidhiano ya mizinga ya nyuki 85 iliyotengenezwa na jeshi la Magereza ambayo itatumika kufugia nyuki katika Mkoa wa Dodoma. Makabidhiano hayo yalifanyika katika viwanja vya Gereza Kuu Isanga, mjini Dodoma. PIX 3.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk Rehema Nchimbi akitoa hotuba kwa maafisa wa Jeshi la Magereza kabla ya makabidhiano ya mizinga ya nyuki 85 iliyotengenezwa na jeshi hilo. Katika hotuba ake hiyo, Dk Nchimbi alimshukuru Mkuu wa Jeshi hilo nchini. Kamishna Jenerali John Minja kwa msaada huo mkubwa ambao utawahamasisha wakazi wa Mkoa wa Dodoma waweze kufuga nyuki. Makabidhiano hayo yalifanyika katika viwanja vya Gereza Kuu Isanga, mjini Dodoma. (Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.)
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top