Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

RC SADICK: ZOEZI LA USAFI JIJINI DAR ES SALAAM NI ENDELEVU

 


SaidiMeckSadickNa Baraka Mpenja wa Fullshangwe Dar es salaam 
Uongozi wa jiji la Dar es salaam  umesisitiza nia yake ya  kusafisha jiji hilo licha ya watu wengi kuamini kuwa zoezi hilo lilitiliwa mkazo zaidi wakati wa ziara ya siku mbili ya Rais wa Marekani, Barrack Obama. 
Hayo yameelezwa na mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Mheshimiwa, SAID MECK SADIC, wakati akizungumza na baadhi ya vyombo vya habari nchini mapema leo asubuhi, ambapo ameweka wazi mipango ya serikali kuendeleza usafi katika jiji, huku akisisitiza kuwa tayari ameshakutana na viongozi wake kupanga mikakati hiyo.
“Sisi tumejipanga sawasawa, usafi sio mpaka waje wageni, hapana kwa kweli! nimeshakaa na Meya wajiji na viongozi wengine na kukubaliana kuongeza juhudi zaidi za kulisafisha jiji letu”. Alisema Mheshimiwa Sadick. 
SADICK aliongeza kuwa ujio wa Mheshimiwa Obama sio sababu pekee iliyosababisha serikali ya mkoa huo kusafisha jiji, bali walikuwa na mipango hiyo kabla ya ujio wa ugeni huo mzito kwa Taifa, na bahati nzuri zoezi likaboreshwa zaidi baada ya ziara ya Rais wa Marekani kuwepo. 
Aidha SADICK aliwataka watu wanaopotosha Umma kuwa nguvu ya serikali ya kusafisha jiji ni nguvu ya soda, bali amewaomba wananchi kutoa ushirikiano mkubwa ili kuliweka jiji katika hali ya usafi tofauti na siku za nyuma. 
SADICK alisisitiza kuwa kama kuna mtu ana amini kuwa zoezi hilo ni nguvu ya soda, basi ajaribu kwenda kinyume na taratibu zilizowekwa na uongozi, na baada ya hapo hiyo nguvu ya soda itaonekana.
Hata hivyo, SADICK alisema suala la usafi ni muhimu kwa afya ya binadamu, hivyo ni wajibu wa kila mkazi wa jiji kutambua hilo na kukubali kutunza mazingira ili aepukane na magonjwa mbalimbali. 
Siku za karibuni, jiji la Dar es salaam ambalo linapondwa na watu wengi kuwa chafu limebadilika ghafla na kuwa safi kufuatia serikali kulisafisha kwa juhudi zaidi wakati wa ujio wa Rais wa Marekani Barrack Obama.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top