KOCHA
David Moyes anajiandaa kukutana na Wayne Rooney na wawakilishi wake kwa
mazungumzo kesho, hilo likiwa jukumu lake la kwanza kubwa tangu aanze
kazi Manchester United.
Mkataba
wa miaka sita wa Mscotland huyo umeanza rasmi leo na atakwenda makao
makuu ya klabu, Carrington kutatua sakata la muda mrefu la Rooney kutaka
kuondoka.
Moyes
anataka Rooney abaki, lakini anafahamu mchezaji huyo mwenye umri wa
miaka 27 aliyesajiliwa kwa Pauni Milioni 25.6 mwaka 2004 anataka
kuondoka.
Tingisha: Wayne Rooney alikuwa kwenye tamasha la muziki Glastonbury mwishoni mwa wiki
Chini ya utawala mpya: Moyes anashikilia mustakabali wa Rooney Old Trafford
Inafahamika
mwanasoka huyo wa kimataifa wa England amejenga fikra zake kwamba
kubadilisha klabu ni njia nzuri kufufua makali yake kuelekea Fainali za
Kombe la Dunia majira yajayo ya joto.
Zaidi itategemea na mazungumzo yake na Moyes ambaye anafanya jitihada za kumbakiza.
Arsenal
na Chelsea zote zinamfuatilia na zina ya kumsajili Rooney na ikiwa
United itakubali kumuuza watalazimika kumuacha ajiunge na moja ya
wapinzani wao katika Ligi Kuu England.
Kama
Rooney atataka kuondoka, United pia inaweza ikataka ada ya uhamisho ya
kiasi cha Pauni Milioni 35, ambazo Paris Saint-Germain na Real Madrid
zinaweza kutoa kununua huduma ya mpachika mabao huyo.
Kocha
wa Real, Carlo Ancelott ni shabiki wake, lakini kumfikiria Rooney
itategemea na Mtaliano huyo mipango yake ya kuwasajili Luis Suarez wa
Liverpool na Edinson Cavani wa Napoli itakuwaje.
Arsenal
wako tayari kuvunja rekodi yao ya usajili na kumfanya pia Rooney awe
mchezaji anayelipwa zaidi kwa kiasi cha mshahara wa Pauni 170,000 kwa
wiki, ambacho ni cha chini kutoka Pauni 225,000 anazolipwa kwa sasa.
Moyes anatakiwa kumaliza suala hili mapema ikiwa anataka kumpata mbadala sahihi.
Aatashughulikia
nyongeza ya dau la kutaka kumsajili beki wa kushoto wa Everton,
Leighton Baines Pauni Milioni 15 na mazungumzo rasmi na Barcelona kuhusu
usajili wa Pauni Milioni 17 wa kiungo Thiago Alcantara.
Mkataba mkubwa: Wayne Rooney atajadili mustakabali wake huku Arsenal na Chelsea zikimsikilizia
Bayern
Munich, Manchester City na Real Madrid nazpo zinafuatilia pia sakata
hilo. Monaco itamfuata Patrice Evra iwapo dili la Baines litakamilika na
timu hiyo ya Ufaransa pia bado inamtaka winga Mreno wa United, Nani.
Kadhalika,
suala la AC Milan kutaka kumsajili Nemanja Vidic limetupiliwa mbali na
wakala wake, Silvano Martina aliyesema: "Vidic hana tatizo United,
yanayozungumzwa yote ni uvumi,".
Wakati huo huo, Arsenal ofa yake ya Pauni Milioni 6 kwa kiungo wa Lyon, Clement Grenier, mwenye umri wa miaka 22 imepigwa chini.
CREDIT: bIN ZUBEIRY BLOG
CREDIT: bIN ZUBEIRY BLOG
Post a Comment