Mshindi
wa Redds Miss Temeke 2013, Sviona Nyameyo (katikati), ambaye ni
mwanafunzi wa mwaka wa kwanza wa Sheria Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
(UDSM), akiwa na mshindi wa pili, Narietha Boniface, mwanafunzi wa
Chuo Kikuu cha Sayansi ya Tiba Muhimbili (MUHAS), na mshindi wa tatu,
Latifa Mohamed ambaye ni muhitimu wa kidato cha sita baada ya kutangazwa
washindi katika shindano hilo lililofanyika viwanja vya Sigara
Chang’ombe Dar es Salaam jana Mshindi

Chang’ombe Dar es Salaam jana
Wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kutangaza washiriki walioingia kwenye kumi bora ya Redds Miss Temeke jana.
…………………………………………………………………………
Na Mwandishi Wetu
MREMBO
Sylona Nyameyo jana usiku alifanikiwa kutwaa taji la Redd’s Miss Temeke
lililofanyika katika Ukumbi wa TCC Changombe, jijini Dar es Salaam.
Sylona
aliye mwanafunzi wa mwaka wa kwanza katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
(UDSM), akisomea mambo ya sheria alifanikiwa kuwashinda warembo wengine
na kufanikiwa kujitwalia taji hilo.
Katika
shindano hilo lililokuwa na upinzani mkali, ulioambatana na burudani za
kumwaga, ilishuhudiwa nafasi ya pili ikienda kwa Marietha Boniface,
ambaye naye ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Tiba Muhimbili
(MUCHS).
Nafasi
ya tatu ilikwenda kwa Latifa Mohammed ambaye amemaliza kidato cha sita
mwaka huu, hivyo warembo hao kujihakikishia nafasi ya kuingia katika
fainali za Redd’s Miss Tanzania.
Ushindani
ulionekana dhahiri katika shindano hilo, ambapo warembo walikuwa
wakichuana mno, huku mashabiki waliojitokeza hapo wakijikuta
wakishangilia muda wote.
Akizungumza
mara baada ya kuvikwa taji hilo, Sylona alisema amefurahishwa mno na
matokeo hayo na atahakikisha hawaangushi wakazi wa Temeke katika
shindano la Redd’s Miss Tanzania.
“Nilijua
toka mwanzo lazima niwashinde, maana nilijiamini na niliona nina vigezo
vyote, sasa ni wakati wa kwenda kupambana katika Redd’s Miss Tanzania
ili kurudisha heshima ya Temeke,” alisema.
Shindano
la Redd’s Miss Tanzania kwa sasa linadhaminiwa na kinywaji cha Redd’s
Original kinachozalishwa na kusambazwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL).
Post a Comment