Mbunge
wa Jimbo la Kitope ambae pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
Balozi Seif akikabidhi Seti ya TV Flat Screen kwa Timu ya Soka ya Mwache Alale
United baada ya kuibuka na ushindi wa godi 5 – 3 dhidi ya African Boys
ya Upenja kwenye mchezo wa Fainal ya Kombe wa Zaweda.
Nahodha
wa Timu ya Soka ya Mwache Alale Abdullghani Gullan akipokea kikombe
kutoka kwa Mbunge wa Jimbo la Kitope Balozi Seif Ali Iddi mara baada ya
timu yake kuibuka na ushindi wa 5-3 dhidi ya African Boys ya Upenja. Pambano hilo lilichezwa katika uwanja wa Kitope na kushuhudiwa na Mbunge huyo Balozi Seif. Picha na Hassan Issa wa –OMPR – ZNZ.
************************
Hatimae
Timu ya Soka ya Mwacha Alale United imeibuka na ubingwa wa mashindano
ya Kombe la Zaweda ndani ya Jimbo la Kitope baada ya kuilaza Timu ya
African Coast ya Upenja kwa mabao 5 – 3 yaliyopatikana kwa njia ya
Penalti katika pambano la fainali lililochezwa kwenye uwanja wa Kitope.
Pambano
hilo lililokuwa na ushindani mkali kwa timu zote mbili lilichezwa kwa
dakika 90 bila ya mshindi lilishuhudiwa na wapenzi kadhaa wa mchezo wa
soka wakiongozwa na Mbunge wa Jimbo la Kitope Balozi Seif Ali Iddi.
Mabingwa
hao wapya wa Kombe la Zaweda Mwache Alale United walifanikiwa kupata
ushindi huo baada ya kufunga Penalti zote tano wakati wapinzani wao
African Boys ya Upenja wakapata Penalti tatu na kupoteza moja.
Mgeni
rasmi wa pambano hilo Mbunge wa Jimbo la Kitope Balozi Seif alikabidhi
zawadi kwa bingwa wa mashindano hayo, mshindi wa pili pamoja na zawadi
kwa timu zote zilizoshiriki katika mashindano hayo ambayo ni ya pili
kufanyika tokea kuanzishwa kwake mwaka uliopita.
Balozi
Seif aliwakabidhi mabingwa wa Kombe hilo Mwacha Alale United Seti moja
ya TV, King’amuzi chake, shilingi 300,000/- taslimu, seti moja ya jezi,
mpira pamoja na Kikombe cha ubingwa.
Mshindi
wa Pili African Boys ya Upenja ikakabidhiwa shilingi laki 150,000/-
Taslimu, seti moja ya jezi, pamoja na mpira wakati mshindi wa Tatu
Mahonda Kids wakaibuka na Seti moja ya jezi, shilingi 75,000/- taslim
pamoja na Mpira.
Mchezaji
bora na mdogo kuliko wote katika mashindano hayo alikuwa Said Khamis
Kidagaa aliyepata zawadi ya shilingi 20,000/- taslimu na Mfungaji bora
wa mashindano hayo Abdull Nyafu wa African Coast ya Upenja alipata
zawadi ya shilingi 20,000/-.
Mchezaji
bora wa mashindano hayo Ali Alawi na Golkipa bora Siad Abdulla kutoka
Timu ya Zaweda wamepata zawadi ya shilingi 20,000/- taslimu kila mmoja
wakati zawadi ya shilingi 50,000/- Taslimu kwa timu bora katika
mashindano hayo ilichukuliwa na timu ya soka ya Zaweda.
Muamuzi
bora wa mashindano hayo aliibuka Haroun Kuchi aliyefanikiwa kupata
zawadi ya shilingi 20,000/- taslim pamoja na mpira mmoja mmoja kwa kila
timu ilizoshiriki katika mashindano hayo.
Timu
zilizoshiriki mashindano hayo ya Zaweda Cup ni pamoja na Mbuyuni,
Fujoni Boys, Mahonda Union, Kitope United,Zaweda, Mgambo F.C, Kilimani
City, Kibweni Youth Organization, New Star, Mahonda Kids,washindi wa
Pili African Boys ya Upenja na Mabingwa wa mashindano hayo Mwacha Alale
United.
Mapema
Mbunge huyo wa Jimbo la Kitope Balozi Seif alikabidhi zawadi kwa
washindi wa mchezo wa Pete wanawake ambapo bingwa ni watanashati wa
Kitope waliopata shilingi laki 100,000/- Taslimu, Mpira pamoja na Seti
ya Jezi.
Mshindi
wa pili wa mchezo huo wa netball ni timu ya wanawake ya kiwengwa
iliyozawadiwa shilingi laki 100,000/- Taslimu, Mpira na Seti ya Jezi.
Akizunguma
mara baada ya pambano hilo la fainal na zawadi Mbunge huyo wa Jimbo la
Kitope Balozi Seif aliwakumbusha wana michezo nchini kuendelea
kushikamana katika michezo ili kuleta upendo michezoni na ndani ya
Jamii.
Balozi
Seif aliwatahadharisha wanamichezo hao kuvitumia viwanja vya michezo
kwa mnasaba wa kiungwana na ustaarabu na kuacha tabia ya kuvifanya
viwanja hivyo kuwa ni maeneo ya kuporomoshwa kwa matusi.
“
Haipendezi kuona maeneo ya viwanja vya michezo nchini yanakuwa sehemu
ya kuporomoshwa matusi ambayo mara nyingi huelekezwa kuwakashifu
viongozi wanaowaongoza wanamichezo hao “. Aliasa Balozi Seif.
Aliwapongeza
Wanamichezo pamoja na uongozi wa Kamati ya mashindano hayo ya Zaweda
Cup kwa juhudi zao zilizosaidia kukamilisha mashindano hayo kwa amani
na furaha.
Jumla
ya shilingi Milioni 2,700,000/- zimetumika kugharamia vifaa mbali mbali
vya mashindano hayo ya Zaweda Cup katika ununuzi wa TV, jezi mipira
pamoja na kikombe.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
Post a Comment