Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI “PRESS RELEASE” TAREHE 08. 07. 2013.


[BARAKAEL MASAKI - ACP]
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

WILAYA YA MBEYA MJINI - MAUAJI
 MNAMO TAREHE 07.07.2013 MAJIRA YA USIKU HUKO MTAA WA MBATA JIJI NA MKOA WA MBEYA. ODEN S/O MKUMBWA, MIAKA 60, MNDALI, MLINZI BINAFSI MKAZI WA NONDE ALIUAWA KWA KUKATWA MAPANGA SEHEMU MBALI MBALI ZA MWILI WAKE NA MTU/WATU WASIOFAHAMIKA AKIWA KAZINI KATIKA LINDO AMBALO NI DUKA LA MADAWA MUHUMU [PHAMACY] LILILOPO ENEO HILO. MBINU ILIYOTUMIKA NI  WATUHUMIWA KUMVIZIA MAREHEMU AKIWA KATIKA LINDO NA  KUMUUA KISHA KUVUNJA DUKA HILO LA DAWA MUHIMU NA KUIBA DAWA ZA  AINA MBALIMBALI PAMOJA NA FEDHA TASLIMU TSHS 600,000/=. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA.. KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA  KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI BARAKAEL MASAKI  ANATOA  WITO  KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU YA  MAHALI WALIPO  WALIOHUSIKA NA TUKIO HILI WAZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI HATUA ZA KISHERIA DHIDI YAO ZICHUKULIWE.
WILAYA YA RUNGWE - AJALI YA GARI KUMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU NA
                                                       KUSABABISHA KIFO.
MNAMO TAREHE 07.07.2013 MAJIRA YA SAA 15:30HRS HUKO ILIMA BARABARA YA MBEYA/TUKUYU WILAYA YA RUNGWE MKOA WA MBEYA. GARI T.654 BPX AINA YA  TOYOTA COASTER LIKIENDESHWA NA DEREVA IMANI S/O MWAKILEMA,MIAKA 34,KYUSA, MKAZI WA KYELA LILIMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU MAGE D/O NSUKEMO,MIAKA 59,KYUSA,MKULIMA ,MKAZI WA ILIMA NA KUMSABABISHIA KIFO CHAKE MUDA MFUPI BAADA YA  KUFIKISHWA HOSPITALI YA  MAKANDANA – TUKUYU KWA AJILI YA  MATIBABU. CHANZO NI MWENDO KASI. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALINI HAPO. DEREVA AMEKAMATWA TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA  KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI BARAKAEL MASAKI  ANAENDELEA KUTOA WITO  KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOENDESHA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUSHA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.
WILAYA YA ILEJE - AJALI YA GARI KUMGONGA MWENDESHA PIKIPIKI NA
                                                    KUSABABISHA VIFO
.
MNAMO TAREHE 07.07.2013 MAJIRA YA SAA 20:00HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA MBEBE WILAYA YA ILEJE MKOA WA MBEYA. GARI NA DEREVA ASIYEFAHAMIKA LILIMGONGA MWENDESHA PIKIPIKI T. 863 BXC AINA YA  SANYA AITWAE OBADIA S/O MWAKIPESILE,MIAKA 36,KYUSA,MKAZI WA MBEBE PAMOJA NA ABIRIA WAKE FRED S/O FUMBIKA,MIAKA 23,MNDALI,FUNDI UJENZI MKAZI WA ISANGA MBEYA NA KUSABABISHA VIFO VYAO PAPO HAPO.  CHANZO NI MWENDO KASI. MIILI YA   MAREHEMU IMEHIFADHIWA HOSPITALINI YA WILAYA YA ILEJE. DEREVA ALIKIMBIA NA GARI MARA BAADA YA TUKIO .KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI BARAKAEL MASAKI. ANAENDELEA KUTOA WITO  KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOENDESHA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUSHA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA. AIDHA ANATOA RAI KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU YA  MAHALI ALIPO MTUHUMIWA  AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE VINGINEVYO AJISALIMISHE MARA MOJA.
Signed By,
[BARAKAEL MASAKI - ACP]
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top