Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

ABDI KASSIM 'BABBI' AIPIGA KIJEMBE AZAM


Na Prince Akbar, - Bin Zubeiry
 
KIUNGO wa kimataifa wa Tanzania, Abdi Kassim Sadallah, maarufu kama Babi au Ballack wa Unguja amesema kwamba hajaachwa na Azam FC, bali yeye mwenyewe alikataa kuongeza Mkataba, licha ya kuombwa mara tatu na uongozi wa klabu hiyo.
Nimewaacha wao; Abdi Kassim
'Babbi' anasema hakuachwa Azam

Hata hivyo, Babi aliyeandika ujumbe huo katika ‘ukuta’ wake wa Facebook, hakusema sababu za kukataa na wala kuhusu mipango yake ya baadaye, zaidi ya kusema atatoa taarifa zaidi baadaye. 
“Naona wengi wananitumia sms..kwa kujua habari za Azam..labda kwa ufupi tu ..niwaambie, kwa urefu nitawambia siku nyengine..mimi sipo Azam. Mkataba wangu umeisha na sikutaka kuongeza, mfahamu hivyo, la kama ningetaka, nigesaini, ila sikutaka, maana nimefanya mazugumzo na Azam mara tatu, hatukuafikiana, mimi hawajaniacha, ila nimewaacha wao,”ameandika Babi.
Babi alijiunga na Azam msimu uliopita akitokea Vietnam alipokuwa anacheza soka ya kulipwa. Kabla ya hapo, Babi alichezea Mtibwa Sugar ya Morogoro akitokea kwao Zanzibar.   Babi alijiunga na Azam msimu uliopita akitokea Vietnam alipokuwa anacheza soka ya kulipwa. Kabla ya hapo, Babi alichezea Mtibwa Sugar ya Morogoro akitokea kwao Zanzibar.   
Babi alikuwa tegemeo la timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars kati ya mwaka 2005 na 2011 na zaidi alikuwa anaibeba timu hiyo enzi za kocha Mbrazil, Marcio Maximo.
Aliweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kufunga bao kwenye Uwanja mpya wa Taifa, Dar es Salaam, Septemba 1, mwaka 2007 wakati Stars ikiilaza 1-0 Uganda katika mchezo maalum wa kirafiki wa ufunguzi wa Uwanja huo.
Sifa yake kubwa ni mashuti makali na ndiyo yaliyomfanya apewe jina Ballack, akifananishwa na kiungo wa zamani wa kimataifa wa Ujerumani na Chelsea, Michael Ballack.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top