Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

ALIYEKAMATWA NA KILO 1,512.69 ZA MADAWA YA KULEVYA AINA YA HEROIN HYHROCHLORID ZENYE THAMANI YA SH68.MIL AFIKISHWA MAHAKAMA YA KISUTU DAR ES SALAAM.

 

MFANYABIASHARA Edson Monyo (39) amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, akikabiliwa na mashitaka  mawili ikiwamo kukutwa na dawa za kulevya zenye thamani ya Sh. milioni 68.

Mshtakiwa huyo alisomewa mashtaka yake mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Hellen Riwa.
 
Wakili wa serikali Leonard Challo alidai kuwa Agosti 4, mwaka huu katika Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere alikamatwa na askari  akiingiza kilo 1,512.69 za dawa za kulevya aina   ya Heroin Hydrochloride zenye thamani ya Sh. 68,069,250.

Katika shtaka la pili ilidaiwa kuwa siku na tarehe ya tukio la kwanza mshtakiwa alikamatwa na askari akiingiza nchini dawa za kulevya aina ya bangi  yenye uzito wa gramu 34.77 yenye thamani ya Sh.13, 908,000.

Wakili Challo alidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.

Hata hivyo, Hakimu Riwa alisema mshitakiwa hatakiwi kujibu chochote kutokana na mahakama hiyo kutokuwa na mamlaka ya kusikiliza kesi ya dawa zenye thamani zaidi ya Sh. milioni 10.

Aidha, kesi hiyo upelelezi wake utakapokamilika itasikilizwa Mahakama Kuu Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam.

Mshitakiwa alikana shtaka la pili la kukamatwa akiingiza bangi nchini.
Hakimu Riwa alisema mshitakiwa apelekwe mahabusu hadi Septemba 3, mwaka huu, kesi hiyo itakapotajwa.
SOURCE: NIPASHE
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top