Habari
zilizoufikia mtandao huu hivi punde kutoka Mkoani Arusha zinaeleza kuwa
Ndege Ndogo ya Shirika la Ndege la TANZAIR iliyokuwa ikitokea Mjini
Bukoba kuelekea Jijini Dar es Salaam, imelazimika kutua katikati ya Ziwa
Manyara lililopo Mkoani Arusha ili kunusuru abiria wake sita (6)
waliokuwamo katika ndege hiyo baada ya kupatwa na hitilafu kwa kuzima
ghafla kwa Injini moja wakati ikiwa hewani.
Aidha
imeelezwa kuwa katika tukio hilo ni abiria watatu tu ambao wamepatwa na
majeraha makubwa huku wakipelekwa kupatiwa matibabu katika Hospitali ya
Sirialni ya Mkoani Arusha, huku wengine wakitazamiwa na kuchunguzwa
kabla ya kuruhusiwa kuweza kuendelea na safari.
Rubani
wa ndege hiyo alilazimika kutaka kutua ghafla katika Uwanja wa Arusha,
kutokana na Hitilafu hiyo, lakini alishindwa baada ya kuona mtikisiko
ukizidi na kuamua kuielekeza ndege hiyo katikati ya Ziwa hilo, ambapo
alifanikiwa kutua salama na baadhi ya Boti na mitumbwi iliyokuwa karibu
iliweza kusogea na kutoa msaada wa kubeba abiria hao na kuwasogeza nchi
kavu na baadaye ilifika Helkopta ambayo iliweza kutoa msaada zaidi.
Kaa nasi kwa habari kamili kadri zitakavyoendelea kutufikia.
Post a Comment