Katibu Mkuu Kiongozi
Balozi Ombeni Sefue anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika tamasha la
michezo (sports bonanza) la uzinduzi wa michezo ya SHIMIWI
litakalowashirikisha Watendaji Wakuu wa Serikali na watumishi wa umma
litakalofanyika siku ya jumamosi Agosti 24 mwaka huu majira ya saa moja
asubuhi katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Hayo
yalisemwa na Kaimu Katibu Mkuu wa Shirikisho la Michezo ya Wizara na
Idara za Serikali (SHIMIWI) Bw. Moshi Makuka akiwa ofisini kwake mapema
leo.
Alisema
dhumuni la michezo hiyo ni kujenga na kulinda afya za viongozi na
watumishi,kuboresha mahusiano kazini,kujenga mshikamano kwa
watumishi,kujenga utaifa na kuondoa tofauti baina ya watumishi.
Alifafanua kuwa bonanza hilo litaambatana na matembezi na mazoezi ya viungo.
“Bonanza
litahusisha matembezi (jogging) kutoka Uwanja wa Taifa kupitia Klabu ya
Sigara,mataa ya Chang’ombe polisi hadi Uwanja wa taifa pamoja na
mazoezi ya viungo yatayoendeshwa na wakufunzi wa michezo”
Aidha,amewahimiza
watendaji wakuu wa Taasisi za Serikali na watumishi wa umma kuhudhuria
tamasha hilo la michezo lililoandaliwa kwa ajili yao.
Kufanyika
kwa tamasha hilo ni utekelezaji wa agizo la Katibu Mkuu Kiongozi na
Mkuu wa Utumishi wa Umma Balozi Ombeni Sefue ambapo aliziagiza taasisi
zote za serikali nchini kushiriki kwenye michezo ili kuimarisha afya
zao.
Post a Comment