Wazo la kuunda baraza la wazee lilitolewa Aprili, 2011 katika kikao cha NEC baada ya wazee kuombwa kutohudhuriwa vikao vya CC kutokana na kuhitaji safari ndefu za mara kwa mara wakati wana umri mkubwa.
Kwa ombi hilo, NEC iliridhia mabadiliko hayo ya katiba wakati wa kikao chake kilichoketi Februari 12, 2012.
Madiwani wa Bukoba kikaangoni
Hatima ya madiwani wanane waliofutiwa uanachama huko mkoani Kagera itafahamika wikiendi hii wakati CC itakapokutana leo. Baada ya CC, kikao cha NEC kitafanyika kesho na keshokutwa.
Nape alisema suala la madiwani wa Bukoba litakuwa miongoni mwa ajenda za kikao cha CC.
Halmashauri ya CCM, Mkoa wa Kagera hivi karibuni iliwafukuza uanachama madiwani hao kutokana na kushirikiana na wale wa Chadema na CUF kupinga uongozi wa Meya wa Mji wa Bukoba, Anatory Amani.
Waliofukuzwa ni Richard Gaspar (Miembeni ), Murungi Kichwabuta (Viti Maalumu), Alexander Ngalinda ambaye pia ni Naibu Meya (Buhembe), Yusuf Ngaiza ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya (Kashai), Deusdedit Mutakyahwa (Nyanga), Robert Katunzi (Hamugembe), Samwel Ruhangisa (Kitendaguro) na Dauda Kalumuna (Ijuganyondo).
Baada ya kufukuzwa, Sekretarieti ya CCM ilitoa taarifa kupinga hatua hiyo ikisema Halmashauri ya Mkoa wa Kagera haikuwa na madaraka ya kuwatimua madiwani hao.
Ajenda nyingine
Nape alisema ajenda nyingine za CC zitakuwa kujadili maoni ya wanaCCM juu ya rasimu ya Katiba, hali ya kisiasa na masuala ya utumishi. Alisema NEC itajadili ajenda moja tu ya maoni ya rasimu ya Katiba Mpya.
Post a Comment