Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi akizungumza na madiwani wa CCM wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma wiki iliyopita.
Katika
hali inayothibitisha ule usemi wa mwanamuziki Chamilion wa Uganda kuwa
“fitina yako bahati yangu” wapinzani wamechezea kichapo cha mwaka kwenye
Halmashauri ya wilaya ya Kibondo baada ya CCM kushinda kwenye nafasi
zote za kuongoza Halmashauri hiyo, ushindi uliowaacha midomi wazi
wapinzani waliokuwa wakisubiri kufaidi kwenye ugomvi wa madiwani wa CCM
wilayani hapo.
Diwani
wa CCM Ndugu Emily Msanya kuibuka Mwenyekiti wa Halmashauri baada ya
kupata kura 14 kati ya 17 zilizopigwa na Makamu Mwenyekiti ni Apronary
Mazinda ambaye pia alishinda kwa kura 14 kati ya 17.
Kuchaguliwa
kwa madiwani hao na ushindi huo wa CCM kwenye ngome ya upinzani ambapo
Mbunge wa jimbo hilo ni Ndg. Mkosamali wa NCCR-Mageuzi ni uthibitisho
dhahiri kuwa CCM ina mkakati mkubwa wa kuzidhibiti ngome zote za
upinzani nchini kuelekea uchaguzi wa 2014 na 2015.Kabla ya uchaguzi huo palikuwa na mgogoro mkubwa kati ya madiwani wa CCM, mgogoro ambao ulitatuliwa na Katibu wa Itikadi na Uenezi Ndg. Nape Nnauye kufuatia ziara yake ya kimyakimya ya siku moja wilayani Kibondo ambapo alikutana na madiwani hao wa CCM kwa zaidi ya masaa manne.
Matokeo
haya ni kinyume kabisa na kile kilichoandikwa na Gazeti la Tanzania
Daima la Agosti 7,2013 kuwa ‘ WIKI NGUMU KWA CCM” wakieleza kuwa CCM
wangepoteza uchaguzi huu. Fitina hiyo ya TanzaniaDaima imegeuka kuwa
bahati kwa CCM maana imetembeza kichapo cha haja kwenye uchaguzi huo.
Nape
akiongea juu ya ushindi huo akinukuliwa na redio moja ya Mjini Mwanza
alisema “ushindi huo ni mawingu mvua zenyewe zinakuja. Unajua hawa jamaa
wanawekeza kwenye migogoro ndani ya CCM ili ikitokea hatukuelewana
mahali basi wanazamia, hapa nimewazidi akili” alikaririwa Nape.
Post a Comment