Kamanda wa Mkoa wa kipolisi wa Temeke, Engelbert Kiondo
********
Kamanda wa Mkoa wa kipolisi wa Temeke, Engelbert Kiondo, alisema wizi huo ulifanyika juzi majira ya kuanzia saa 1:00 hadi saa 3:30 usiku kwenye ghala la Al Naem Enterprisses eneo la Mbagala Rangitatu, mali ya Harun Zakaria.
Watu hao (majina yao hayakutajwa), walifanikiwa kufanya uhalifu huo baada ya kuwazidi nguvu walinzi wanne waliokuwa wakilinda kwa kuwapiga kwa mapanga, kisha kuwafunga kamba na kuwafungia chooni.
Kamanda Kiondo, alieleza kwamba kabla ya kuingia ndani ya ghala, majambazi hayo yaligonga geti na kujifanya wanataka kuingiza mzigo ndani, ndipo mlinzi mmoja alipofungua mlango waliingia kundi la watu 10 na kutembeza kipigo kwa walinzi hao.
"Hawa majambazi walipofika waliigiza sauti ya mmoja wa wafanyakazi wanaopeleka mizigo pale kwenye ghala, walinzi waliposikia sauti ile walifungua mlango," alisema Kamanda Kiondo.
Alisema waliiba mifuko 1,312 yenye ujazo wa kilo 50 kila moja na kupakia ndani ya lori.
Katika purukushani ya kuwakamata, majambazi hayo yalitoa rushwa ya Sh. milioni 30 kwa ajili ya kuwafanya waruhusiwe kuendelea na safari yao.
"Vijana wetu wa kituo cha Mbagala hawakukubali kupokea pesa hiyo, tumewakamata na tunafanya jitihada ya kuwafikisha mahakamani muda wowote baada ya kukamilika kwa uchunguzi.
Akizungumzia afya za walinzi hao, Kamanda Kiondo, alisema mlinzi mmoja amelazwa Hospitali ya Temeke baada ya hali yake kuwa mbaya kutokana na kuvunjika mkono na wengine wanaendelea vizuri.
CHANZO:
NIPASHE
Post a Comment