NA MWANDISHI WETU
CHAMA Cha Michezo ya Jadi Tanzania
(CHAMIJATA) kimewaomba wadau wa michezo kujitokeza kukisaidia chama
hicho shilingi milioni 40 ili kufanikisha mashindano ya Taifa ambayo
yanatarajiwa kufanyika jijini Dar es Salaam kuanzia Septemba 20 hadi 24
mwaka huu.
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa CHAMIJATA Mohamed Kazingumbe wakati akizungumza na mwandishi wa habari hii jijini Dar es Salaam.
Alisema
mashindano hayo ambayo yatashirikisha mikoa yote ya Tanzania Bara na
Visiwani ni moja ya utaratibu wa chama hicho kufanya michezo ya jadi
kila mwaka kwa lengo la kukuza tamaduni za nchi.
Kazingumbe
alisema katika mashindano hayo wanatarajia kuwa kutakuwa na michezo
mbalimbali kama bao, kurusha mshale, mdako, mirela, kukuna nazi na
mingine mingi ambayo itakuwa ikitambulisha michezo ya jadi nchini.
“Tunatarajia
kufanya mashindo ya michezo ya jadi ya Taifa kuanzia Septemba 20 hadi 24
ila mpaka sasa changamoto kubwa ambayo inatukabili ni fedha hivyo
tunaomba wadau wenye kupenda michezo hii wajitokeze kusaidia,” alisema.
Alisema hadi
sasa ni mikoa michache imethibitisha kushiriki ambayo ni Pwani, Simiyu,
Lindi, Morogoro, Dar es Salaam pamoja na baadhi ya taasisi za Serikali
ila bado mikoa mingine inaendelea kuonyesha nia ya kushiriki.
Mwenyekiti
huyo alisema mikoa ambayo bado haijathibitisha kushiriki inatakiwa
kufanya hivyo hadi ifikapo Agosti 30 mwaka huu ambapo maandalizi mengine
yatakuwa yanendelea.
Kazingumbe
alisisitiza kwa vyama vya mikoa na wilaya kuhakikisha kuwa vinafanya
mandalizi ya kutosha ili kuhakikisha kuwa ushindani unakuwa mkubwa na
kuleta tija.
Aidha alivitaja vyama vya michezo ya jadi na mikoa kuhakikisha kuwa wanashirikiana ili kufanikisha mashindano hayo
Post a Comment