Mwenyekiti
wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akiongoza kikao maalum cha Kamati Kuu ya
CCM, Makao Makuu ya CCM, mjini Dodoma leo, Agosti 25, 2013. Kikao hicho
kilifanyika kwa ajili ya kukutana Mbunge wa Bukoba mjini Khamis
Kagasheki, Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kagera, Constansia Buhiye, Katibu
wa CCM mkoa wa Kagera Abedi Mushi, Mwenyekiti na Katibu wa CCM wilaya ya
Bukoba mjini na Meya wa Manispaa ya Bukoba Anatory Amani, kuhusu
mgogoro wa madiwani wanane wa CCM Manispaa ya Bukoba. Kulia ni Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana. Mwenyekiti
wa CCM mkoa wa Kagera Constansia Muhiye na Katibu wa CCM wa mkoa huo,
Abedi Mushi wakisubiri kuingia ukumbini kukutana na Kamati kuu mjini
Dodoma leo.
Mbunge wa Bukoba mjini Khamis Kagasheki akiwasili Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma.
Kagasheki akiingia ukumbini
Karibu
wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akimsikiliza kwa makini
Mwana-CCM mwenye ulemavu wa miguu, Shija Luhende kutoka Mwanza, ambaye
alimkuta kwenye viwanja vya Makao Mkuu ya CCM mjini Dodoma leo,
akitafuta msaada wa baiskeli. (Picha na Bashir Nkoromo).Mwenyekiti
wa Jumuia ya Wazazi ambaye pia ni mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM,
Abdallah Bulembo akizungumza na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Jenista
Mhagama, nje ya ukumbi, Makao Mkuu ya CCM mjini Dodoma, leo
Post a Comment